Mkuu wa Nchi hana huruma kwa raia wa hali ya chini? Hali ya Chakula nchini ni mbaya

Mkuu wa Nchi hana huruma kwa raia wa hali ya chini? Hali ya Chakula nchini ni mbaya

Debe la mahindi linacheza kwenye elfu 22.

Kipunga na maharage ndio kipepaa vibaya sana. Leo hii mchele ni sh 3000 na maharage elfu 3000.

Mkuu wa nchi yupo kimya na anachukulia poa tu.

Wananchi wa kawaida hawana uhakika wa kula

Wakati analima Wewe una Bet
 
Nyie wehu tulieni.
Mlipiga kelele kuwa 70%-75 % ni wakulima.
Sasa Rais kaonyesha utu kwa wakulima ili waneemeke kwa kuuza mazao yao bei nzuri mnakasirika.
Mlikuwa mnaona raha kununua MAHINDI gunia sh. 30000 huku gharama ya kuzalisha gunia moja ni zaidi ya sh. 50000.
Tulieni wendawazimu nyie.
 
Mnataka kuwa control wakulima kwa sababu zipi?
Hao wakulima wanapolima huwa mnawapa mbolea bure? Mnawapa maji ya kumwagilia? Mnawapa matretka au kuwasidia kushika jembe shambani?
Kwa akili yako uliona ni sahihi waachwe wauze mazao bila control ili maharage tununue elfu 4 kama ilivyo sasa
 
Aliyekuwa na huruma ndiye aliwaambia serikali haina shamba kwa hiyo hatawaletea chakula.

Bora hata mama ana huruma kuliko lile dereva la lori aina ya tipa lenye mawe
 
Nyie wehu tulieni.
Mlipiga kelele kuwa 70%-75 % ni wakulima.
Sasa Rais kaonyesha utu kwa wakulima ili waneemeke kwa kuuza mazao yao bei nzuri mnakasirika.
Mlikuwa mnaona raha kununua MAHINDI gunia sh. 30000 huku gharama ya kuzalisha gunia moja ni zaidi ya sh. 50000.
Tulieni wendawazimu nyie.
Huu ndio muda mkulima atafurahia maisha, serikali imefanya jambo jema
 
Hii nchi ni kama Barcelona tu.. ni mwendo wa kuuza economic levers ili tufanikiwe sasa, ya baadae yatajijua
 
Debe la mahindi linacheza kwenye elfu 22.

Kipunga na maharage ndio kipepaa vibaya sana. Leo hii mchele ni sh 3000 na maharage elfu 3000.

Mkuu wa nchi yupo kimya na anachukulia poa tu.

Wananchi wa kawaida hawana uhakika wa kula
ulitaka aingie shambani akalime ndo ujue ana anachofanya?
mbona kuna ambaye alikaa miaka 5 bila kupandisha watu mishahara wala madaraja hatukuwasikia mkibweka? au watumishi wa umma siyo wananchi? samia kawapandisha na mambo yapo poa
kamfufue magufulia aje aseme chochote juu ya mchele kupanda bei?
unajua sababu kuu zinazochangia vyakula kupanda bei lakini?
nsije nikawa naongea na form four
 
Unajua kunawakati ili watu wajitume lazima vitu vya muhimu kama chakula lazima vipande bei, haiwezekani mtu apate wali maharage kwa jero au buku alafu uniambie watu watajituma. Mtu anakupiga kizinga cha miatano anaenda kula msosi masaa yanaenda ikifika jioni anapiga kazi ya sarange anapata buku mbili anakula msosi wa buku na bangi mbili tatu alafu useme taifa litapata watu wachapakazi.
 
Mnataka kuwa control wakulima kwa sababu zipi?
Hao wakulima wanapolima huwa mnawapa mbolea bure? Mnawapa maji ya kumwagilia? Mnawapa matretka au kuwasidia kushika jembe shambani?
Pembejeo na mbolea walinunua bei gani na sasa ni bei gani?
 
Back
Top Bottom