Tetesi: MKUU WA NCHI KUWAONDOA BAADHI YA MAWAZIRI

Tetesi: MKUU WA NCHI KUWAONDOA BAADHI YA MAWAZIRI

Status
Not open for further replies.

kilaza mjanja

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2016
Posts
654
Reaction score
1,144
Taarifa zilizo tufikia kupitia vitengo vyetu vya udukuzi wa taarifa upo mpango wa kuwaondoa baadhi ya mawaziri walipo kwenye baraza la mawaziri walioshindwa kuendesha wizara zao kwa ufanisi.

Baada ya kushambuliwa baadhi ya mawaziri bungeni hapa ikulu vikao haviishi kuhusu namna ya kulisuka upya baraza la mawaziri ambalo linasadikiwa kukosa mvuto kwa wabunge na jamii kwa ujumla.

Japo swala hili linajadiliwa kwa usiri mkubwa ila mpaka sasa wapo baadhi ya mawaziri wameshaitwa ikulu kuhojiwa juu ya utendaji wao na wengine kuandikiwa barua za onyo wa mwenendo wao.

Pia mjadala mwingine uliopo ikulu ni ule wa mgogoro mzito ulipo kati ya waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mh lukuvi na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ambao umeonekana kubeba sura ya kuiaibisha serikali kwa massage alio tuma mh lukuvu kwa paul makonda ya kusema "wewe ni nani kwenye serikali hii? mbona unaingilia majukumu yasiyo yako?" ambapo kiupitia ujumbe huo ulisababisha kurushiana maneno baina ya viongozi ndani ya serikali hii.

Tamati, ni kweli vipo vikao vya tasmini juu ya baraza la mawaziri na baadhi ya viongozi wa serikali hii ya awamu ya tano, muda sio mrefu mbeleni mambo yatakuwa wazi.

by
kilaza mjanja wa magogoni
 
Juzi kajibu vizuri swali la tido leo hii awaondoe
any ways tunajia kusimamia kauli ni ngumu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom