Tetesi: MKUU WA NCHI KUWAONDOA BAADHI YA MAWAZIRI

Tetesi: MKUU WA NCHI KUWAONDOA BAADHI YA MAWAZIRI

Status
Not open for further replies.
Paul Makonda amelewa sana sifa na limbukeni wa kutupwa... yule kijana hana adabu kabisa na uwepo wake DSM unaondoa credibility ya Magufuli kwa jamii.
 
Atabadilisha mpaka mwaka 2020.
kisu cha ngariba,
Andika kiswahili fasaha tukuelewe! 'Atabadilisha' au 'Hatabadilisha'?
Mbona tayari alishabadilisha Mambo ya ndani kwa kumtoa Kitwanga na kumwingiza Mzee Madelu Nchemba??Je, hilo siyo badiliko? Mimi nataka nikuhakikishie kuwa mpaka kufikia 2020 Mawaziri wengi watautema Uwaziri kwa kupenda au kutopenda!
Time gonna tell and I am ready to bet for that!! Scandal iliyoibuliwa juzi na KUB kuhusu rushwa ya 10m kwa kila Mbunge wa CCM lazima iondoke na watu! Kuna kufilisika kwa Benki ya Twiga Bankcorp, JPM amesema kuna Wanasiasa wamekomba Mabilioni ya fedha kati ya 5B-20B na hawa ni wana CCM na JPM atalala nao mbele we subiri tu!
 
Taarifa zilizo tufikia kupitia vitengo vyetu vya udukuzi wa taarifa upo mpango wa kuwaondoa baadhi ya mawaziri walipo kwenye baraza la mawaziri walioshindwa kuendesha wizara zao kwa ufanisi.

Baada ya kushambuliwa baadhi ya mawaziri bungeni hapa ikulu vikao haviishi kuhusu namna ya kulisuka upya baraza la mawaziri ambalo linasadikiwa kukosa mvuto kwa wabunge na jamii kwa ujumla.

Japo swala hili linajadiliwa kwa usiri mkubwa ila mpaka sasa wapo baadhi ya mawaziri wameshaitwa ikulu kuhojiwa juu ya utendaji wao na wengine kuandikiwa barua za onyo wa mwenendo wao.

Pia mjadala mwingine uliopo ikulu ni ule wa mgogoro mzito ulipo kati ya waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mh lukuvi na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ambao umeonekana kubeba sura ya kuiaibisha serikali kwa massage alio tuma mh lukuvu kwa paul makonda ya kusema "wewe ni nani kwenye serikali hii? mbona unaingilia majukumu yasiyo yako?" ambapo kiupitia ujumbe huo ulisababisha kurushiana maneno baina ya viongozi ndani ya serikali hii.

Tamati, ni kweli vipo vikao vya tasmini juu ya baraza la mawaziri na baadhi ya viongozi wa serikali hii ya awamu ya tano, muda sio mrefu mbeleni mambo yatakuwa wazi.

by
****** mjanja wa magogoni
Ikulu hakuna wapuuzi kama wewe
 
Makonda ni mpiga dili Sana, chai yake iko mezani tutamlipua muda sio mrefu

Michezo anayoshirikiana na meya wa jiji la Dar es salaam tunayo yote, hata michezo na wafanyabiashara tumeidaka yote

Makonda subiria chai Yako iko jikoni
 
Orodha Imekamilika Wababaishaji Hawatapona
Kwa Wahariri Jumanne Pondamali Mensah
Aliona Haya Akameza Maneno Tu
Ila Sasa Baraza Linakwenda Kubomolea Na Watakaondoka Tutawataja Soon!
 
List hii hapa

1:- January Makamba

2:-Muhongo

3:-J4 Maghembe


Na mengine ntawaletea kadri nnavyopenyezewa
 
Lukuvi ni potential Sana kuliko hata huyo makonda, viongozi wanaingilia majukumu mengine hayawahusu, lazima kuwe na mipaka
Hata Kama Makonda alikosea lakini kauli aliyotumia Lukuvi sio ya hekima.Ni ya kujikweza na kibabe.
 
Asante kwa taarifa ila nenda tena kwenye semina ya uandishi ili ujifunze namna ya kutumia herufi kubwa na herufi ndogo. Kumbuka, majina ya watu, miji, nk huanza kwe herufi kubwa...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom