Mkuu wa Shule na Mzazi wa Mwanafunzi walinitengenezea zengwe hadi nikafukuzwa kazi

Mkuu wa Shule na Mzazi wa Mwanafunzi walinitengenezea zengwe hadi nikafukuzwa kazi

Kwa mtazamo wangu kuna Jambo umeficha kwenye story yako. Mgogoro ni mwepesi wa wewe kukufikisha kwenye hatia ya kukufukuza kazi. Labda kama uelewa wangu ni mdogo.

Unafundisha somo gani? Maisha ya ualimu sio serikalini tu hata private yapo tena yaweza kuwa mazuri kuliko huko endapo una umahiri mkubwa kwenye somo lako.
unakuta kafukuzwa ualimu na utumishi yaan vyeti vimefungiwa
 
Ndio mkuu. Kwa madai yake amesingiziwa kumtaka huyo mwanafunzi na mwalimu mkuu akishirikiana na mzazi na mwanafunzi wamefanikisha kutengeneza ushahidi uliowezesha kumfukuza kazi.

Swali ni Kwanini mwalimu mkuu apate ushirikiano kutoka kwa mzazi na mwanafunzi kumuumiza mtu ambaye tangu wanamfahamu amekua akiwatendea wema na wamefanya hayo akiwa anajaribu kuwasaidia hitaji lao ambalo lilikuwa linakwamishwa na huyo huyo mwalimu mkuu?
Aise! haya maswali ni magumu
 
Kweli. Kama kaonewa atafanikiwa tu kimaisha hata kama si hapo shuleni na waliomuonea watapata kazi ya kujisafisha kwake. Hii imetokea mara nyingi.
kweli mkuu japokuwa wanasema dua la kuku halimpati mwewe basi tena
 
Hakuna kesi ya kufukuzwa kazi kwa ushahidi wa kufikirika na mwepesi kama huo hata kama ni kweli ulimtongoza huyo binti. Labda kama ungekuwa umemtafuna kweli, na ukakamatwa na vielelezo/vidhibiti vya kutosha! Mfano ujumbe mfupi kwenye simu, umekutwa naye ndani ya chumba chako na huyo mwanafunzi, umempa ujauzito, nk.

Wewe endelea kupigania haki yako. Ikiwezekana nenda kwa DAS, RAS, nk kutoa malalamiko yako. Na baada ya hapo fanya utaratibu wa kuomba kuhamia shule iliyo kwenye Kata/Tarafa nyingine ndani ya hiyo Halmashauri yako ili kuepukana na hizo changamoto.
kweli hata wanaoua japo ushahidi unakuwepo mbona wanahamishwa tu
 
Inaonesha wewe mwl ulikuwa karibu na huyo mwanafunzi, kuna shida mahali haiwezekani kila kiongozi awe against wewe
wakati mwingine yaweza kuwa au mama mzazi mbona alikuwa anapambana na mkuu wakati kashika makali
 
1.. umewahi kuwa karibu na huyo bint?
2. Mara ngapi amekuwa akiuza duka lako au wakati gani?
3. Kama ulikuwa msaada kwa mama na baba wa mtoto imekuaje nao wakugeuke ikiwa hakukuwa na nia yoyote ovu kwa mtoto?
Duu! sema tu kabla halija kupata unaweza usijue 𝐏𝐈𝐀 𝐇𝐀𝐏𝐀 𝐊𝐔𝐍𝐀 𝐊𝐄𝐒𝐈 𝐘𝐀 𝐀𝐉𝐈𝐑𝐀 𝐘𝐀 𝐙𝐀 𝐖𝐀𝐓𝐎𝐓𝐎
 
Umeoa? Ungekuwa na ndoa mke ndo angekuwa bullet proof yako ya Kwanza kuwa huna nyege mlipuko.....sasa mtu ukute hujaoa, halafu unacheka Cheka na mwanafunzi, unamtuma nyumbani kwako, unamtuma dukani, unamnunulia madaftari, unampambania hadi unakorofishana na mkuu wako.....huyo mwanafunzi mwenyewe anaweza kuhisi unamtaka[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Ushauri wangu ukifanikiwa kurudi kazini acha kujenga bifu na mkuu wako, akikutafuta hakukosi as hujakamilika.....ishi kinafiki, usiulize ulize mambo ya pesa, hayakuhusu.....
pambana na mishe zako kimya kimya.....sio umefungua kimradi kimekubali unawaona staff wenzio hawajielewi wewe ndo una akili..... watu wakilia njaa na wewe lia njaa, kwenye ualimu wachawi ni wengi.....Kama staff ina walimu 20, ujue wachawi hawapungui 17[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
𝐡𝐚𝐡𝐚𝐡𝐚
 
Hakuna haki nchi hii kama ni hivyo, inawezekanaje niwatreat wenye matatizo na wasiokuwa na matatizo the same?
Kwamba ilibidi nimuache mtoto mwenye shida ya Usajili kwa kuwa tu ni binti?
Changamoto sana!
𝐖𝐞𝐧𝐠𝐢𝐧𝐞 𝐰𝐚𝐥𝐢𝐨𝐩𝐨 𝐦𝐚𝐠𝐞𝐫𝐞𝐳𝐚𝐧𝐢 𝐬𝐢 𝐤𝐰𝐚𝐦𝐛𝐚 𝐰𝐚𝐧𝐚𝐡𝐚𝐭𝐢𝐚 𝐛𝐚𝐥𝐢 𝐰𝐚𝐥𝐢𝐬𝐢𝐧𝐠𝐢𝐳𝐢𝐰𝐚
 
Suala la uhusiano na imani yako ya kimapenzi kati yangu na huyo mama ni imani unayoiamini wewe, mimi sikuwahi kuwa na huo uhusiano naye wa kimapenzi huyo mama, na nimeweka wazi kuhusu mwalimu aliyemtaka kingono kuwa si mkuu wa shule, KASUMBA ZETU NA TAMAA (Vipaumbele) ZA KIMAPENZI zinawafanya wengi waamini hivyo! Kama msaada wangu ulipelekea hayo POTELEA MBALI, NILIOWAFUNDISHA KWA MIAKA KUMI WALIFAULU NA WANATOSHA NA NITAWASAIDIA WENGINE HATA IKIWA URAINI KADRI YA NITAKAVYOKUWA.
Suala la upande aliokuwepo mama baada ya kuhojiwa kwa njia ya simu maelezo yake yalikuwa upande wa mume wake kwa kuwa taarifa zote alikuwa akiwasiliana na mumewe kwa simu.
Nilikwisha kata rufaa, na nilieleza sababu za rufaa yangu, Nawaelewa sana ushauri wenu, changamoto ni pale mnaponilazimisha nifunguke kitu kisichokuwepo. Au nifunguke nini zaidi?
hapa watu watakushambulia sana bora utafute mwasaikolojia pembeni akusaidie kurudisha akili yako sawa kwanza
 
Watanzania ni watu waoga sana kutetea haki zao. Hivi wewe huoni ubaya wa yeye kukaa kimya bila kulisafisha jina lake? Unajua akikaa kimya na kutafuta shughuli nyingine itakuwa na impact gani kwenye maisha yake ya baadae? Makox usikubali huu ushauri. Hata kama unataka kuachana na ualimu lakini pigana ili ukweli ujulikane.
masuala kama haya yanahitaji raslimali nyingi kama huna hela huwezi endesha kesi mkuu
 
mie nahis mkuu alitaka rushwa katika regstration ya mtoto .ndo hyu ticha akampa mfumo wa siri wakufika ngazi za juu ..mkuu akaona anaharibiwa dili hapo...
Makox hebu clear hapa
Huenda lakini mimi sina uhakika kwa kuwa sikuwahi kuongea chochote uso kwa uso na mkuu wa shule kuhusu tatizo la usajili wa mtoto lakini alichokuwa anakilazimisha kifanywe (Kumlazimisha mtoto akariri au ahame kwa lazima), ni kosa la rushwa pia (Matumizi mabaya ya madaraka).
Na ukweli ni huo kuwa kosa langu lililompa hasira mkuu wa shule ni la mimi kumpa mfumo wa siri wakufika ngazi za juu, (Nina uhakika kwa sababu siku niliyompa ushauri huo mzazi ndiyo mzazi na mtoto walipoanza kuandikishwa barua za malalamiko ya mimi kumtongoza huyo mwanafunzi tena wakiwa ndani ya ofisi ya mkuu wa shule pasipokuwa na mtu mwingine wa ziada.
 
Walimu wengi hujipendekeza na kuacha majukumu yao ya msingi.
Utasikia tu...mrudi wikiendi/jioni niwafundishe....mara mkanichotee maji nyumbani.
Hujifanya wako na uchungu na wanafunzi kuliko wazazi wenye wa wanafunzi.
Hili huwatengenezea mazingira ya kazi kuwa hatarishi.
Na limewaponza wengi.
🤔
 
Yaani asingiziwe na kufanyiwa unayambisi namna hiyo halafu ashukuru Mungu? Unatania? Apiganie haki yake hata ikibidi mpaka Mbinguni. Hii nchi tumezoea mambo ya kujidanganya kuwa eti ''tunaachia Mungu'' na kufanya mabaya yazidi kumea. Mungu haachwi mambo ambao una uwezo nayo.
NIPO TAYARI KUPAMBANA NA YEYOTE KATIKA HILI, KAMA YUPO WAKUNIUNGA MKONO NAMUOMBA SANA KWA MIKONO MIWILI.
 
Back
Top Bottom