Mrs Besyige
JF-Expert Member
- Aug 27, 2019
- 1,040
- 2,923
word!...Mara nyingi ukiwa na huruma/roho nzuri matokeo yake ni kuumizwa tu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
word!...Mara nyingi ukiwa na huruma/roho nzuri matokeo yake ni kuumizwa tu.
Kama ni kweli,shukuru Mungu kwa kilichokutokea.Kuna kiongozi mmoja wa serikali amewahi kuniambia hivyo pia.
Hakika nimeona balaa lake, furaha yao ya pamoja ni kuona mkienda pamoja kukopa pesa, vyombo, mashuka, nyama na bidhaa madukani tena kwa riba kubwa na siyo mtu kujishughulisha!
Nilikuwa na duka ndani ya shule kisheria, nimewahi kuvunjiwa inasemekana kwa njama za walimu nikaibiwa lakini nilipambana nikaendelea, baadaye nikaongeza miradi mingine binafsi ya kuniingizia pesa kama kuuza chipsi, mishkaki, juisi na vitafunwa, walipoona biashara inasonga mbele wakaniwekea mazingira magumu sana nikafunga kibanda😭😢 Haikupita muda ndiyo likatokea hili mkuu hivyo naamini Walimu wanaishi maisha ya uadui sanaaaaa. Bado unaenda kwa AEK, CWT, na TSC Unakuta wote ni walimu tena wenye maisha ya kuungaunga tangu kwenye elimu zao😁😅😸
Walimu wengi hujipendekeza na kuacha majukumu yao ya msingi.Kwa ubishi huu sasa unaona unachokutana nacho? Walimu wa kiume wapo ukaribu wako na mwanafunzi unaishia Darasani, Shuleni.
Wewe unapata wapi mamlaka ya kumfanya mwanafunzi auze duka lako? Huo ukaribu unautoa wapi? Ni mwanafunzi wa Day?
Una undugu naye?
Umemwajiri?
Ulipata kibali toka kwa wazazi wake?
Je tunajuaje hukuwa na mahusiano naye ya kimapenzi? Wewe kazi yako kufundisha masomo darasani au kufundisha wanafunzi wa kike kuuza duka?
Ungekuwa unafundisha Maths na Physics usingepata muda wa kupiga stori na mke wa mtu. Pole kwa yaliyokukuta ila ni ngumu sana TSC kufikia hatua ya kumfukuza kazi mwalimu.sipo tayari kuficha chochote ili nipewe msaada mkuu. Nafundisha English mkuu
unamfahamu alie kuajili...?Nimenyoosha kwa kiwango changu cha juu kabisa kiongozi
Pole mkuuMimi ni Mtanzania mwezenu, nimeandika na kuweka katika jukwaa hili ili niweze kujengewa uwezo na ushauri na yeyote atakayeguswa na habari yangu; kama kuna sehemu haitaeleweka nipo kwa ajili ya ufafanuzi. Tafadhari siyo sawa kutumia lugha za matusi, kejeli na dharau kwani kila mtu ana changamoto yake.
Nimekuwa mtumishi wa Serikali katika kada ya ualimu tangu 2013-2023 mwezi wa tano. Nikiwa katika utekelezaji wa majukumu yangu nimekutana na changamoto nyingi sana za kawaida ambazo ni muhimu kazini.
Changamoto iliyonileta hapa ni hii sasa ambayo ni hatari kwa maisha yangu, familia yangu na jamii kwa ujumla.
Nilianza kanzi katika kituo xx, nikiwa huko nilikuwa karibu sana na mfanyakazi mmoja Askari wa Maliasili, nikiishi naye vizuri mpaka nahama kule mwaka 2017. Kwa bahati mbaya yule askari alikuja kupata changamoto za kiafya na akili na hivyo kupelekea familia yake kuyumba sana na hatimaye ndoa yake kuvunjika.
Mwaka 2022 january, nikiwa naendelea na majukumu nilikutana na Mke wa rafiki yangu(Yule Askari) akiwa amekuja shuleni kufuatilia taratibu za kumhamishia pale mtoto wake aliyetakiwa kuanza kidato cha kwanza shule niliyokuwa nafundisha awali, alifurahi sana kuniona kwani hakufahamu kama nilihamia pale. Baada ya kusalimiana alinijulisha juu ya changamoto alizopitia mpaka ndoa kuvunjika na tayari alikuwa ameolewa na mtu mwingine hatimaye tukaja kwenye changamoto ya uhamisho wa mtoto wake.
Kwa maelezo yake alifanikiwa kupewa namba za simu za makamu mkuu wa shule ili aweze kuomba nafasi, kwa bahati mbaya alipewa majibu kuwa nafasi zimejaa lakini atampatia namba za mwalimu mwingine ajaribu kuongea naye. Mama baadae alitumiwa namba hizo na kufanya mawasiliano na mwalimu huyo.
Majibu ya mwalimu yalikuwa Ahadi ya kupatikana kwa nafasi endapo mama [mzazi] atafanikiwa kuwapata watoto wengine angalau watatu ili wawe wanne na watatakiwa kulipia nafasi hizo kwa Tsh.20000 ili jumla iwe 80000. Majibu ya mzazi ilikuwa haiwezekani kutokana na ugeni wa mazingira na kutokufahamu ni nani mwenye uhitaji huo kwa haraka.
Basi yule mwalimu akamtaka mzazi atoe 50000 kwa ajiri ya nafasi ya mtoto. Kutokana na ugumu wa maisha ilionekana pesa kuwa ni nyingi mno, wakakubaliana kulipana 40,000/=, Lakini kadri muda ulivyozidi kwenda bado haikuwezekana kupatikana kwa pesa hiyo. Baada ya kuona hivyo mzazi ilibidi atoe taarifa hiyo kwa huyo mwalimu. Mwalimu aliyapokea majibu na kuamua kubadirisha masharti hayo na kumtaka yule mzazi kingono kwa siku tatu mfululizo ili ampatiye nafasi.
Kwa mujibu wa mzazi ilikuwa ni vigumu kwake kukataa na kukubali pia, lakini kutokana na uhitaji wake alikubali kufanya hivyo ili mtoto apate haki nafasi ya masomo, japo aliamini kuwa ingemuathiri sana kisaikolojia.
Hivyo siku niliyokutana naye pale shuleni ni siku aliyohitaji kuja kuonana na mwalimu kwa kuwa hawakuwahi kuonana.
Baada ya kunipa maelezo hayo nilimwuliza kama anamfahamu angalau kwa jina, akasema hamfahamu. Nikaamua kuomba namba yake, ilikuwa ni ngeni kwangu, lakini baada ya kuangalia kwenye mtandao wa M-Pesa niligundua kuwa ni namba ya mwalimu niliyemfahamu.
Kwa kumsaidia yule mama nikamwambia yule mama namfaham mwalim huyo, na nikaahidi kumuunganisha naye kwa masharti kuwa amwambie hayupo tayari kuwa naye kingono, ila ampe hiyo nafasi ya mtoto na kuhusu pesa amwambie aje achukue kwangu. (Nilisema hivyo kwa kuwa nilijua kuwa asingeweza kuja kunidai pesa hiyo, kwani alitambua kuwa mimi nilikuwa najihusisha na masuala ya kuzuia na kupambana na Rushwa shuleni hapo nikiwa ni Mlezi wa Klabu ya wanafunzi).
Kwa bahati nzuri baada ya wawili hao kukutana na mzazi kutoa maelezo hayo, Mwalimu alishtushwa sana kuona mzazi akinitaja, alilalamika na hatimaye kumwambia yule mzazi ameharibu utaratibu wao, hivyo amlete mtoto hivyo hivyo aje aanze masomo.
Nilipewa mrejesho wa mazungumzo hayo na yule mzazi, nilifurahi kwani kilichokuwa kikihitajika pale ni nafasi ya masomo na kuzuia rushwa. yote yaliwezekana.
Kuhusu kumleta mtoto shule maandalizi yalikuwa yamefikia hatua nzuri isipokuwa kulikuwa na upungufu wa daftari 4 counter book quire 2. Kwa kuzingatia ukaribu wa mzazi huyo na mimi, nilianua kucgukua daftari nne dukani kwangu na kumkabidhi yule mzazi ili mtoto aanze masomo yake kwa wakati.
Kweli mtoto kesho yake aliletwa tayari kuanza masomo na muda wote nilikuwa naye karibu kama mtoto wangu.
Alisoma kidato cha kwanza kwa mahudhurio mazuri bila kufanya kosa lolote la kinidhamu Japo kwa upande wa utawala walikuwa wakisua sua sana kukamilisha uhamisho huo mtandaoni wakidai Hawana PREM-NUMBER ya mwanafunzi huyo. Baada ya kupewa taarifa hiyo kwa haraka nilishughulikia na uhamisho ukakamilishwa.
Mwaka 2023 Shule zilifunguliwa na mwanafunzi aliendelea na masomo yake ya kidato cha pili. Kutokana na utaratibu wa shule ilikuwa wanafunzi wa madarasa ya mitihani ni lazima wakae kwenye kambi zilizoandaliwa shuleni baada ya kukamilisha michango yao. Mwenzi wa pili mkuu wa shule alitangaza kuwa wanafunzi wote wasiohamia kambini waende wakafuate mahitaji kwa wazazi wao.
Mwanafunzi wangu naye akaondoka akaenda kufuata michango hiyo, kwa bahati mbaya ilikuwa ni wiki ya mwisho wa Usajili kwa ajili ya mitihani ya kidato cha pili, hivyo akiwa hajarudi shuleni wezake walipigwa picha kwa ajili ya usajili huo.
Siku ya mwisho ya usajili nilipewa taarifa ya kukosekana kwa picha ya mwanafunzi huyo na kuwa ilikuwa siku ya mwisho ya usajili. Baada ya kupewa taarifa niliamua kufanya mawasiliano na mzazi, ili ampige picha na anitumie ili niwakabidhi waweze kumsajili.
Hatukufanikiwa kupata picha siku hiyo kwani kule kijijini hakukuwa na mtu mwenye simu kubwa (Simu janja).
Niliamua kumtaarifu mwalimu aliyekuwa akishughulikia usajili huo, nikaambiwa mfumo umeshafungwa hivyo mwanafunzi itabidi akariri darasa.
Nilimpa taarifa baba mlezi wa mtoto(MAMA ALIKUWA AMESAFIRI) naye akaniomba nimshauri nini afanye ili mtoto asajiliwe. Baada ya kazi nilimtafuta akanielekeza kwake nikaenda kufanya mazungumzo ya kumsaidia mtoto. Tulikubaliana mimi nifuatilie kwa ngazi ya hapo shuleni ili utawala waone jinsi gani wanatatua tatizo hilo.
Niliwasilisha ombi ofisi ya Taaluma, na Mtaaluma akalipokea na kwenda kuliwasilisha kwa Mkuu wa Shule, Kwa bahati mbaya majibu ya mkuu wa shule yalikuwa Mimi niache kufuatilia tatizo la mtoto kwa madai kuwa hanihusu.
Nilipokea mrejesho huo kwa huzuni kubwa sana kutokana na mazingira halisi ya mtoto yule na kumtaarifu baba mlezi wa mtoto kwa kuwa wakati huo Mama mzazi alikuw nje ya mkoa kwa shughuli za kifamilia.
Baba mlezi aliendelea kufuatilia huku tukipeana ushauri kwa ukaribu mkubwa. Siku moja mlezi akiwa ofisini kwa mkuu wa shule ilionekana Mkuu wa Shule anamshauri mlezi amkaririshe mtoto baada ya kwenda kwa daktari wakatengeneze vielelezo vya kuthibitisha kuwa mtoto hakusoma vizuri kidato cha kwanza kutokana na kuumwa sana. Mzazi alikuwa tayari kwa hilo lakini mwanafunzi hakutaka kurudia kidato kimoja akiamini ni aibu kwa wanafunzi aliokuwa akisoma nao. Hivyo mkuu wa shule akasema basi itabidi wamhamishe aende akakariri katika shule nyingine.
Mlezi alinitumia taarifa ya mazungumzo hayo kwa njia ya ujumbe wa simu huku akiwa ndani ya osisi ya mkuu wa shule. MAJIBU niliyoyatoa ilikuwa ni mlezi kuomba ruhusa kwa mkuu wa shule kama usajili hauwezekani kwa ngazi ya shuleni basi aruhusiwe afanye mawasiliano na Katibu Tawala wa Mkoa au Baraza la mitihani, Mlezi akakubali na kuniomba nimpatie namba za watu hao atakapotoka ofisini.
NDUGU WANA JAMVI, HAPO NDIPO ULIKUWA MWANZO WA TATIZO. Siku hiyo ndipo mawasiliano yangu na mlezi yalipokoma na kesi zangu kuibuliwa ghafla. Nakumbuka hiyo ilikuwa ni tarehe 16/03/2023 nilipomshauri mzazi aombe ruhusa ya kufanya mawasiliano na ofisi za juu.
Tarehe 17/03/2023 mzazi aliitwa shuleni na mkuu wa shule na kuambiwa aandike barua ya kulalamika kuwa mimi nimekuwa nikimtongoza mtoto wake tangu alipoanza kidato cha kwanza na kumtumia kama mwuza duka wangu baada ya kusoma. Mzazi aliandika barua hiyo akithibitisha kuwa aliyafahamu mahusiano hayo,
Mtoto naye akaandikishwa barua kuwa nilikuwa nikimtongoza sana na kumpiga viboko vingi alipokuwa akinikataa.
TAREHE 20/03/2023 Mkuu wa Shule aliwatuma Walimu wa Nidhamu na Malezi wanihoji nikaitikia wito na kuhojiwa.
TAREHE 21/03/2023 Nilipewa barua na mkuu wa shule akitaka nijitetee kuwa sina mahusiano ya kimapenzi na mwanafunzi huyo, niliipokea barua hiyo na kuijibu.
Baada ya siku chache nikaambiwa na mkuu wa shule nahitajika ofisi wa Afisa Elimu wa Kata (Mratibu kata), nilienda kule ofisini na kukuta wananisuburi ndani ya ofisi ya Afisa Mtendaji wa Kata na Afisa Mtendaji Kata akiwa ndiye mwenyekiti wa mazungumzo akiwa na Mkuu wa Shule na Mratibu. Alitumia nguvu sana kunilazimisha nikiri kumtaka kimapenzi mwanafunzi yule, sikuweza kukubali kwa kuwa haikuwa kweli. Mtendaji kata alipiga simu Polisi kumtaka askari aje aniweke chini ya ulinzi, baada ya Askari kufika na kupewa maelezo alihitaji ampate atakayekuwa mlalamikaji wa Kesi hiyo, Wote Watatu wakakataa na hivyo nikarihusiwa niondoke.
Baada ya wiki moja niliitwa na TSC Wilaya, nikapewa Notes na Hati ya Mashitaka tuhuma ikiwa ni “KUWA NA TABIA YA MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA MWANAFUNZI YANAYOASHIRIA KUTAKA KUFANYA NAYE TENDO LA NDOA).
Nilijibu na kuiwasilisha kwa wakati, waliunda tume ya uchunguzi wakaja kunihoji, na kuwahoji baadhi ya mashahidi mbele yangu, na wengine kwa njia ya simu.
JAMBO LA KUSHANGAZA waliandikishwa barua za maelezo kwa siri na kuambatanisha kwenye muhtasari wa mahojiano. Na yule mwanafunzi alikuwa ameshahamishwa hivyo mkuu wa shule akalazimishwa amsafirishe aje kuhudhuria mahojiano. Na mkuu wa shule akamwagiza mhasibu ahakikishe mwanafunzi huyo anasafirishwa tena kwa pesa ya shule.
Siku chache baadae niliitwa Tena ofisi ya TSC WILAYA NA KUPEWA BARUA YA KUFUKUZWA KAZI.
Kwa barua ile nilikata rufaa tangu mwezi July 2023 lakini mpaka sasa sijajibiwa kwa madai kuwa mpaka Raisi afanye uteuzi wa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu Makao Makuu.
POLENI SANA NDUGU WANAJUKWAA KWA KUWACHOSHA NA MAELEZO HAYO MAREFU!
Aidha Nategemea kupata Ushauri na Misaada yenu ndugu zangu Nisije nikaishia kuwa Kichaa.
Stori imebadilika ghafla nimeshindwa kuunga doti. Mpaka ifike hatua ya mzazi kughairisha hitaji muhimu la maendeleo ya kielemu kwa mwanaye na kuandika barua ya kumlalamikia mwalimu kuna kitu hakijawekwa sawaMimi ni Mtanzania mwezenu, nimeandika na kuweka katika jukwaa hili ili niweze kujengewa uwezo na ushauri na yeyote atakayeguswa na habari yangu; kama kuna sehemu haitaeleweka nipo kwa ajili ya ufafanuzi. Tafadhari siyo sawa kutumia lugha za matusi, kejeli na dharau kwani kila mtu ana changamoto yake.

Watanzania ni watu waoga sana kutetea haki zao. Hivi wewe huoni ubaya wa yeye kukaa kimya bila kulisafisha jina lake? Unajua akikaa kimya na kutafuta shughuli nyingine itakuwa na impact gani kwenye maisha yake ya baadae? Makox usikubali huu ushauri. Hata kama unataka kuachana na ualimu lakini pigana ili ukweli ujulikane.jiandae kutafuta kingine cha kufanya kupata riziki, watu waliodhamiria kukuweka sehemu mbaya hawatashindwa kuendelea kuhakikisha unakuwa pabaya zaidi na zaidi.
ubaya hurudi kwa ubaya na wakati mwingine ubaya unabaki kimya bila marudio ya ubaya wala wema, unaweza kuwatarajia hao waliokufanyia hayo wakutane na malipo ya ubaya wao lakini ikawa kinyume chake, badala yake wewe ndie unae umia.
maoni yangu achana nao, tafuta kingine cha kufanya hauta aibika .
Mwaswali mazuri ya kuanzia. Ila mwalimu mkuu anaonekana yupo kwenye mkondo wa mwalimu aliyedai ngono/fedha.Unadhani kwanini mwalimu mkuu ametumia njia katili na ya kukuchafua kukuondoa kazini huku akijua huna hatia?
Unadhani kwanini mzazi wa mwanafunzi aliafiki kuwa upande wa mwalim mkuu ilihali ulikuwa unamsaidia binti yake na mwalimu mkuu hakuwa upande wa kumpa msaada?
Achana na naye. Hizi thread watu wanaandika katika mazingira magumu na pengine wanatumia simu hivyo mambo ya kuzingatia paragraph na sijui nini inakuwa vigumu.Lakini ndiye anayefundisha mpaka watu wanaelewa jinsi ya kuandika aya.
Hata hivyo asante kwa mchango wako
Mkuu Makox achana na tapeli huyo. Narudia tena huyo jamaa ni tapeli anayekifanya anajua kuloga. Atakupiga na kukumalizia fedha zako zote bila huruma na hutapata suluhisho. Usijaribu kabisa.Nakuomba inbox ndugu
Wewe una akili ya kuchambua mambo.Nakubaliana nawewe mkuu. Hapo pia sijaona pccb kuhusika.
Ila mjue hawa watu wapo wanaroho mbaya sana.
Nashauri ukiwaunauhakika mwanamke ana ushahidi japo kwa kesi hii mumewe atakuwa amempiga mkwara hevi akae mbale nawe ama sivyo atamuacha na mwanawe.
Kwa namna nilivyoelewa mwanamke alifiwa akaoelewa..naona pia aliolewa harakansana baada ya ndoa ya kwanza kutetereka. Inaonekana mwanamke ni mdhaifu kupindukia
Sikubliani na maoni yako. Nadhani wewe huna empathy ndiyo maana unaandika hivi. Kwenye maisha binadamu tunatakiwa tusaidie pale tunapoona wenye shida. Huyu jamaa alifanya jambo zuri sana na ni mfano wa kuigwa.Nimesoma andiko lako lote nimegundua udhaifu mkubwa kwenye hii kesi yako na hao wakubwa zako. Anyways msaada wako ulitakiwa kuishia tu kwa kumuelekeza mzazi (huyo Mama) kwa watawala ama wahusika ili afuatilie kila kitu mwenyewe kuanzia kwenye issue ya uhamisho wa binti mwenyewe. Kulichukua hilo jambo na kulifanya kama lako ama wewe ndo mzazi wa huyo binti ama mume wa huyo Mama ndo shida ilipoanzia. Wema una mipaka yake na kua makini na kufanya wema kwa mtu ambao una athari hasi kwa watu wengine specifically wakubwa zako. Kitendo cha kumwambia huyo Mama akareport hilo swala kwa katibu tawala kwako uliona ni msaada ila ulikua unawachomea utambi na kuwaharibia kazi wakubwa zako kitu ambacho wasingeweza kukubali kirahisi na hapo inamaana tayari ulikua ushaanzisha vita. Mbaya zaidi vita yako inahusisha mwanamke (huyo Mama) na mbaya kuliko vyote inahusisha mwanafunzi wa kike underage [emoji725] halafu uko kwenye kada ya elimu/ ualimu ambapo kimaadili na kiutumishi inakubana sana ukihisishwa na jambo hilo. Sijui kama kuna vitu umeficha lakini kama ulichoeleza ndo ukweli ulivyo basi fuatilia ngazi za juu hata Wizarani utachomoka tu japo itachukua muda ila haki yako itapatikana. Kwa maisha ya sasa acha kila mtu ahangaike na watu/ familia yake maswala ya kujifanya mwema sana tena wema wenyewe unahusisha mwanamke/ mtoto wa kike utaharibu tu future yako Mzee.
Yaani asingiziwe na kufanyiwa unayambisi namna hiyo halafu ashukuru Mungu? Unatania? Apiganie haki yake hata ikibidi mpaka Mbinguni. Hii nchi tumezoea mambo ya kujidanganya kuwa eti ''tunaachia Mungu'' na kufanya mabaya yazidi kumea. Mungu haachwi mambo ambao una uwezo nayo.Kama ni kweli,shukuru Mungu kwa kilichokutokea.
Achana na hiyo kazi isiyo na marupurupu.
Pambana kivingine utatoboa for sure.
stress zinaweza kukufanya upige nyeto.mkuu we hujui tu kwakuwa halija kufika sali sanaMwalimu Ni mwalimu tu
Just imagine mwalimu anashindwa kuandika kwa Aya