Mkuu wa Shule na Mzazi wa Mwanafunzi walinitengenezea zengwe hadi nikafukuzwa kazi

Sikuweza kufanya hivyo kutokana na jinsi jambo lilivyoendeshwa mkuu, ilikuwa ni ghafla sana na kimya kimya likaenda wilayani na kutolewa maamuzi magumu. Hata wananchi wamebaki wanashangaa mpaka sasa maana sijawahi kuvutana na yeyote miaka sita nikiwa hapo. Na nilikuwa ni mjumbe wa bodi ya ushauri ya shule
Kuna kitu kikubwa unakikosa cha ushawishi na kujipambania, hata mchungaji wako, hata wazee wa kanisa seriously, ntabaki nasoma comments tu
 
Duuuuh.
Hata Kwa kusoma tu kisa chako, na mimi nimepata maswali mengi.

Je ni wanafunzi wote na wazazi wote unawa treat the same na huyo binti na huyo mama?

Mazingira yanakufunga.
 
1.. umewahi kuwa karibu na huyo bint?
2. Mara ngapi amekuwa akiuza duka lako au wakati gani?
3. Kama ulikuwa msaada kwa mama na baba wa mtoto imekuaje nao wakugeuke ikiwa hakukuwa na nia yoyote ovu kwa mtoto?
 
Kwa ambao tunazurura kutafuta tunakubali inawezekana imetokea lakini kuna kitu kinatufanya tusikubali moja kwa moja.

Mkuu wa Shule ghafla tu aamue kufanya hivi. Anapata faida gani wewe kufukuzwa? Anapata hasara gani wewe kubaki?

Binafsi kama ningetaka kumsaidia huyo mama ni ningempa ile 50K au ningeongea na makamu.
 
Mh maelezo yanatia uwalakini kidogo. Iweje watu wote hao wakubaliane kirahisi na uongo wa mkuu wa shule?
Kuanzia mzazi, mwanafunzi, mratibu, afisa elimu na tcs? Hata walimu wenzio wanaojua ukweli walishindwa kabisa kupenyeza taarifa kwa wahusika au ndo wote hao walipangwa na mkuu wa shule au wote hao wana chuki? Kufukuzwa kazi serikalini siyo ishu rahisi hata kidogo kuna jambo nyuma ya pazia ambalo hauko tayari kuliweka wazi
Unafukuzwa TU kirahisi kama hauana uwezo wa kujitetea na hauna mbuyu juu watu Wana roho mbaya hatari.
 
Nenda tume ya maadili,pana taasisi inayosikiliza malalamiko ya watumishi kabla ya mahakama ,japo haya mambo ya rufaa uchukua miaka Bora upambane na mengine ukiwa unasubiria rufaa Yako,ukishindwa pote huko,tambua Mungu kakupangia riziki ingine.
 
Umeoa? Ungekuwa na ndoa mke ndo angekuwa bullet proof yako ya Kwanza kuwa huna nyege mlipuko.....sasa mtu ukute hujaoa, halafu unacheka Cheka na mwanafunzi, unamtuma nyumbani kwako, unamtuma dukani, unamnunulia madaftari, unampambania hadi unakorofishana na mkuu wako.....huyo mwanafunzi mwenyewe anaweza kuhisi unamtaka🤣🤣🤣

Ushauri wangu ukifanikiwa kurudi kazini acha kujenga bifu na mkuu wako, akikutafuta hakukosi as hujakamilika.....ishi kinafiki, usiulize ulize mambo ya pesa, hayakuhusu.....
pambana na mishe zako kimya kimya.....sio umefungua kimradi kimekubali unawaona staff wenzio hawajielewi wewe ndo una akili..... watu wakilia njaa na wewe lia njaa, kwenye ualimu wachawi ni wengi.....Kama staff ina walimu 20, ujue wachawi hawapungui 17🤣🤣🤣🤣
 
Nimesoma kwa furaha sana comment yako, ina mawazo makubwa sana. Nimeoa na ninaishi na mke. Sijawahi kumtuma mtoto nyumbani.
Unafiki wa staff ni kitu kikubwa sana nakiona hapa. Nimekuelewa pia kwa Ushauri mkuu
 
Kwa jinsi uvyoeleza na nikitathmini nguvu, mali, moyo na akili ulivyotumia kumpambania huyo mwanafunzi kuanzia uhamisho hadi kutokurudia darasa ni dhahiri kuwa ulikuwa una mfaidi mama yake (mke wa rafiki yako). Na kwakuwa mkuu wa shule nae alikuwa anataka amfaidi huyo mama ila wewe ukaweka zengwe, ni lazima angekuundia zengwe tuu, hataka kama ningekuwa mimi (ila siyo kali hivyo).
Pia baba mlezi wa huyo mwanafunzi alijazwa chuki na HM kuwa unamchapia mke wake na akapewa fact kwa namna unavyompambania binti yake nae akajaa king. Hapa hata kama mimi ndo ningekuwa baba wa huyo mwanafunzi, ningeunganisha dots na ningekuundia zengwe tuu.
Mama wa mwanafunzi itakuwa aliwekwa mtu kati huku HM, kule mumewe.....akubali kuachika kwa kesi kuwa unamchapa au aunge mkono hoja kuwa unamzengea binti yao. Jibu rahisi kwa mwanamke yeyote ni kukuangushia jumba bovu ingawa pengine hakujua itafikia stage hiyo kama kweli mlikuwa mnapendana au nawe ulimzingua? Hapo mama hajakuweka wazi yupo upande upi na hujataka kutuambia (TUNAHITAJI JIBU HAPA). Kwa upande wa mwanafunzi ni rahisi sana kupigwa biti kuwa utafukuzwa shule usipokubali kusema kuwa mwalimu alikuwa anakutongoza na kukuhonga visenti na madaftari.

USHAURI WA AWALI:
Kata rufaa na ukiri kuwa ni kesi ya chuki kati yako wewe na HM. Chanzo kikiwa ni wivu wa mapenzi baina yako wewe na mama wa huyo mwanafunzi na HM. Funguka usaidiwe. Hapo kesi itahamia kuwa ya madai baina yako wewe na mwenye mkewake.
 
Sisi watu bhana! Pole sana mkuu ndiyo Dunia hiyo inabidi upambane nayo, wakati mwingine matukio yanakuja ktk maisha hadi unahisi ni mchezo wakuigiza ama? Acha nisign out...
 
Duuuuh.
Hata Kwa kusoma tu kisa chako, na mimi nimepata maswali mengi.

Je ni wanafunzi wote na wazazi wote unawa treat the same na huyo binti na huyo mama?

Mazingira yanakufunga.
Hakuna haki nchi hii kama ni hivyo, inawezekanaje niwatreat wenye matatizo na wasiokuwa na matatizo the same?
Kwamba ilibidi nimuache mtoto mwenye shida ya Usajili kwa kuwa tu ni binti?
Changamoto sana!
 
Sisi watu bhana! Pole sana mkuu ndiyo Dunia hiyo inabidi upambane nayo, wakati mwingine matukio yanakuja ktk maisha hadi unahisi ni mchezo wakuigiza ama? Acha nisign out...
Naamini hivyo
 
Kwa jinsi uvyoeleza na nikitathmini nguvu, mali, moyo na akili ulivyotumia kumpambania huyo mwanafunzi kuanzia uhamisho hadi kutokurudia darasa ni dhahiri kuwa ulikuwa una mfaidi mama yake (mke wa rafiki yako). Na kwakuwa mkuu wa shule nae alikuwa anataka amfaidi huyo mama ila wewe ukaweka zengwe, ni lazima angekuundia zengwe tuu, hataka kama ningekuwa mimi (ila siyo kali hivyo).
Pia baba mlezi wa huyo mwanafunzi alijazwa chuki na HM kuwa unamchapia mke wake na akapewa fact kwa namna unavyompambania binti yake nae akajaa king. Hapa hata kama mimi ndo ningekuwa baba wa huyo mwanafunzi, ningeunganisha dots na ningekuundia zengwe tuu.
Mama wa mwanafunzi itakuwa aliwekwa mtu kati huku HM, kule mumewe.....akubali kuachika kwa kesi kuwa unamchapa au aunge mkono hoja kuwa unamzengea binti yao. Jibu rahisi kwa mwanamke yeyote ni kukuangushia jumba bovu ingawa pengine hakujua itafikia stage hiyo kama kweli mlikuwa mnapendana au nawe ulimzingua? Hapo mama hajakuweka wazi yupo upande upi na hujataka kutuambia (TUNAHITAJI JIBU HAPA). Kwa upande wa mwanafunzi ni rahisi sana kupigwa biti kuwa utafukuzwa shule usipokubali kusema kuwa mwalimu alikuwa anakutongoza na kukuhonga visenti na madaftari.

USHAURI WA AWALI:
Kata rufaa na ukiri kuwa ni kesi ya chuki kati yako wewe na HM. Chanzo kikiwa ni wivu wa mapenzi baina yako wewe na mama wa huyo mwanafunzi na HM. Funguka usaidiwe. Hapo kesi itahamia kuwa ya madai baina yako wewe na mwenye mkewake.
Suala la uhusiano na imani yako ya kimapenzi kati yangu na huyo mama ni imani unayoiamini wewe, mimi sikuwahi kuwa na huo uhusiano naye wa kimapenzi huyo mama, na nimeweka wazi kuhusu mwalimu aliyemtaka kingono kuwa si mkuu wa shule, KASUMBA ZETU NA TAMAA (Vipaumbele) ZA KIMAPENZI zinawafanya wengi waamini hivyo! Kama msaada wangu ulipelekea hayo POTELEA MBALI, NILIOWAFUNDISHA KWA MIAKA KUMI WALIFAULU NA WANATOSHA NA NITAWASAIDIA WENGINE HATA IKIWA URAINI KADRI YA NITAKAVYOKUWA.
Suala la upande aliokuwepo mama baada ya kuhojiwa kwa njia ya simu maelezo yake yalikuwa upande wa mume wake kwa kuwa taarifa zote alikuwa akiwasiliana na mumewe kwa simu.
Nilikwisha kata rufaa, na nilieleza sababu za rufaa yangu, Nawaelewa sana ushauri wenu, changamoto ni pale mnaponilazimisha nifunguke kitu kisichokuwepo. Au nifunguke nini zaidi?
 
Asante kwa ushauri, tume ya maadili ya ngazi ipi mkuu, maana iliyofanya maamuzi ni ya Wilaya, na rufaa nilikata kwenda TSC makao makuu. Samahani naomba unielekeze mkuu.

Back
Top Bottom