Mkuu wa Shule na Mzazi wa Mwanafunzi walinitengenezea zengwe hadi nikafukuzwa kazi

Kama ni kweli,shukuru Mungu kwa kilichokutokea.
Achana na hiyo kazi isiyo na marupurupu.
Pambana kivingine utatoboa for sure.
 
Walimu wengi hujipendekeza na kuacha majukumu yao ya msingi.
Utasikia tu...mrudi wikiendi/jioni niwafundishe....mara mkanichotee maji nyumbani.
Hujifanya wako na uchungu na wanafunzi kuliko wazazi wenye wa wanafunzi.
Hili huwatengenezea mazingira ya kazi kuwa hatarishi.
Na limewaponza wengi.
 
Nikirudi nitamalizia kusoma hii stori,
Ila hadi hapa nilipofika,Kuna mtu alishawahi kupata kesi kama hii ya kwako,Yeye alitengenezewa na Mwalimu mwenzie..binadamu sisi ni balaa.
Ila.alishinda.

Pole Mkuu
 
sipo tayari kuficha chochote ili nipewe msaada mkuu. Nafundisha English mkuu
Ungekuwa unafundisha Maths na Physics usingepata muda wa kupiga stori na mke wa mtu. Pole kwa yaliyokukuta ila ni ngumu sana TSC kufikia hatua ya kumfukuza kazi mwalimu.
 
Pole mkuu
 
Stori imebadilika ghafla nimeshindwa kuunga doti. Mpaka ifike hatua ya mzazi kughairisha hitaji muhimu la maendeleo ya kielemu kwa mwanaye na kuandika barua ya kumlalamikia mwalimu kuna kitu hakijawekwa sawa
 
Watanzania ni watu waoga sana kutetea haki zao. Hivi wewe huoni ubaya wa yeye kukaa kimya bila kulisafisha jina lake? Unajua akikaa kimya na kutafuta shughuli nyingine itakuwa na impact gani kwenye maisha yake ya baadae? Makox usikubali huu ushauri. Hata kama unataka kuachana na ualimu lakini pigana ili ukweli ujulikane.
 
Mwaswali mazuri ya kuanzia. Ila mwalimu mkuu anaonekana yupo kwenye mkondo wa mwalimu aliyedai ngono/fedha.
 
Lakini ndiye anayefundisha mpaka watu wanaelewa jinsi ya kuandika aya.
Hata hivyo asante kwa mchango wako
Achana na naye. Hizi thread watu wanaandika katika mazingira magumu na pengine wanatumia simu hivyo mambo ya kuzingatia paragraph na sijui nini inakuwa vigumu.
 
Wewe una akili ya kuchambua mambo.
 
Sikubliani na maoni yako. Nadhani wewe huna empathy ndiyo maana unaandika hivi. Kwenye maisha binadamu tunatakiwa tusaidie pale tunapoona wenye shida. Huyu jamaa alifanya jambo zuri sana na ni mfano wa kuigwa.
 
Kama ni kweli,shukuru Mungu kwa kilichokutokea.
Achana na hiyo kazi isiyo na marupurupu.
Pambana kivingine utatoboa for sure.
Yaani asingiziwe na kufanyiwa unayambisi namna hiyo halafu ashukuru Mungu? Unatania? Apiganie haki yake hata ikibidi mpaka Mbinguni. Hii nchi tumezoea mambo ya kujidanganya kuwa eti ''tunaachia Mungu'' na kufanya mabaya yazidi kumea. Mungu haachwi mambo ambao una uwezo nayo.
 
Haki ya mtu haipotei kama una uhakika haukumtongoza dogo kweli nicheki pm nikupe code ya mganga utarudi kazini chap ila hakikisha kweli hukumtongoza dogo
 

Attachments

  • 722EE35D-6D1C-46A6-9BF0-9C11CFB7F56E.jpeg
    112.8 KB · Views: 5
Waliokufanyia ubaya watalipwa hasa huyo mtoto hatokaa afanikiwe kwa alichokifanya kwa kusema japo alidanganywa na mzazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…