Mkuu wa Shule ya Sekondari Nyiendo wilayani Bunda jitafakari kama kiti kinakutosha

Presidents office,regional administration and local govt
Mtihani wa kupima uelewa

Part one:Chagua jibu sahihi
Ulipoamua kuondoa walimu 11 na kuwapeleka shule za msingi huku shule yako ikiwa imebaki na walimu wachache,ulifanya hayo ukiwa


A:Umelewa

B:Utatafuta wengine Kwa gharama zako

C:Ulikuwa umerogwa


D:Hukujali maana watoto wako hawasomi shule husika

Na kama jibu ni A,je unatumia kilevi gani?
A:Wanzuki
B:chang'aa
C:mnazil
D:Majibu A,B,C yote ni sahihi

Je baada ya kuondoa walimu shule ikapwaya,lawama zielekezwe Kwa nani?
A:Wewe
B:walimu
C:Wanafunzi
D:Wazazi

Una mkakati gani kuziba pengo la uhaba wa walimu uliolisababisha wewe na kusababisha serikali kulaumiwa pasipo SABABU za msingi?
A:Bado unafikiria
B:Bora liende maana unakaribia kustaafu,msala utamwachia atakayekuja
C:Unasubiri watakaoajiriwa na serikali waletwe tena na serikali
D:Utakuwa unaazima shule jirani





PART TWO:JIBU MASWALI YOTE KAMA ULIVYOULIZWA

5.Eleza dhana nzima ya neno makundi shuleni

6.Kwa Nini baadhi ya wakuu wa shule wanaendekeza makundi shuleni
7.Kwa Nini una tabia ya kuwajengea chuki wakosoaji wako?
8.Je uwajibishwe au usiwajibishwe na Kwa Nini toa SABABU 10
9.Eleza faida tano unazopata shuleni kwa kuondoa walimu wako na kuhamishia shule za msingi
10.Kwa Nini kwenye kikao cha jumatano walimu waligoma kuchangia hoja mpaka ukaweka amri ya Kila mtu achangie kuanzia mtu wa kwanza mpaka wa mwisho?
11.Kwa Nini unapenda kumkejeli Mwenyezi Mungu?
12.Wakati unawaeleza walimu kikaoni utaanza kufuatilia utaratibu na wasianze kukulaumu ulimaanisha tangu uwe mkuu wa shule ulikuwa hufuatilii?Kwa Nini ulikuwa hufuatilii?Kwa Nini unahisi watakulaumu?
Tunataka Nyiendo mpya ambayo Kila mtu

Atakuwa na haki sawa
mtu awajibike
💪Solidarity

Sasa hivi tunaanza kupiga kwenye mshono!Halafu na wewe madame uliyekuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanafunzi wako wa kiume file lako lipo jikoni linamaliziwa,halafu na wewe uliyeigiza kuongea Jana Kwa uchungu Kwa busara za kinafiki tunaandaa file la mkeo na jamaa yake wa chuoni,jiandae kubeba gunia la msumari kichwani!

Tunaanza kupiga kwenye mshono sasa!

Mezani vijana Wana mafaili 12 ya moto ambayo tutaanza kuyadondosha baada ya masaa au siku kadhaa!


Stay tuned
Mjukuu wa kigogo
 
Waweza kuwa na hoja haswa haswa ya kuhamisha waalimu 11 kwenda msingi ila ukiingiza habari za waalimu na mahusiano yao ya chuoni unafeli
 
Mtoa mada anakabiliwa na tatizo kama la Deo Kisandu (sijuwi amepotea wapi sikuhizi).
Na kama ni mwl basi hapo unapofundisha hufanyi kazi,hayo ni majungu tena ya kitoto.
Fuata utaratibu wa kiutumishi katika kutoa malalamiko yako au hoja zako kuliko unachoandika na kuwasagia kunguni wenzako.
 
Ilisikika sauti ya mwl. Mmojawapo aliyeshiriki kikao kikamilifu na kuchangia hoja kwa kulazimishwa na mkuu wa shule
 
Punguza majungu na kufitinisha watu wewe! Wewe itakua ni mjita
 
Sasa wewe kwa uoga huu ulionao Walimu tutatoboa kweli?.. Aisee najuta kua mwalimu,, Kaz hii imejaa vilaza waoga Kama Mwamba huyu!.. Sasa hayo unayosema hapa si ungemchana huyo mkuu kwenye kikao??
 
Mkuu umekula?
 
watumishi wa halmashauri kwa majungu na umbea hamjambo sasa hapa jamii forum ndiyo mamlaka yake ya nidham?
 
hivi wewe mwalimu una Akili timamu?
no wonder ualimu unadhalilisha na kila mtu sijawai kuona upumbavu A list kama huu
 
Sijasoma mpaka mwisho ila We jamaaa kwa uchawi na majungu na fitina shetan anakaa pembeni.

Mwalimu wa aina hii hata kuloga analoga.
 
Kama huyo mwl ni motor na anapg madili yake aachwe Tuu [emoji39]

Huko juu sikuhz hawalambi tena asali Bali wanakula kbsa bila ata kuogopa ,

Kumbuka juu kukioza chin kunanuka[emoji3][emoji58][emoji32][emoji594]


Wew mwl ulieleta taarfa pamban kutafuta ela acha majungu maisha na kaz NI wew mwenyew au UNATAKA CHEO NA WEW NENDA KALOGE[emoji91]
 
Walimu wana matatizo ila ukweli mchungu nikwamba staff za shule za secondary zina majungu na ujuaji kuliko zile za msingi
 
Pale ambapo mwalimu unajifanya mwanaharakati, upo bize kusumbia uongozi unajifanya mchambuzi mpaka umechukua logo ya kigogo eti unajifanya kigogo wa bunda. Kuajiriwa ni utumwa mwalimu unahitaji uwe mnyenyekevu uweze kutoboa. Ukileta uanaharakati wako wa kichuo chuo kutwa unayajengea hoja na kuyajadili maelekezo ya viongozi wako kisa eti una ka digrii hautoboi kwenye utumiahi wa uma
 
Ndugu Mwalimu, mleta mada, embu haya mambo kayafikishe kwa afisa elimu secondary wako.
Huku itaonekana ni majungu na unafiki wako.
 
Summary pliz maana haya ni majungu. Kwani ngazi za kuripoti hazipo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…