TANZIA Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Ukerewe, Masoud Mohamed akutwa hotelini akiwa ameaga dunia

TANZIA Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Ukerewe, Masoud Mohamed akutwa hotelini akiwa ameaga dunia

G Sam

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
11,795
Reaction score
36,704
Kamanda wa Polisi Wilaya ya Ukerewe, Masoud Mohamed amefariki dunia ghafla akiwa ndani ya hoteli.

Afande Masoud alijizolea umaarufu katika mitandao ya kijamii kwa usomaji wa Quran.

Taarifa zaidi kutoka Jeshi la Polisi zitakujia.

9B845506-038A-45B7-B75B-4CEC1FC5A7AF.jpeg

======​
OCCID wa Wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza,Masoud Mohammed amekutwa kafariki sehemu aliyofikia.

Masoud Mohammed ni moja wa Maaskari waliobadilishwa Vituo hivi karibu.

Ukerewe ni kituo chake kipya cha kazi wakati kituo chake cha zamani cha kazi ni Bunda Mkoani Mara.

Masoud Mohammed ndo kwanza alikuwa kapandishwa Cheo cha kuwa OCCID hata hana muda mrefu na kituo chake cha kazi cha kufanya kazi kama OCCID ilikuwa ni hapo Ukerewe.

Alipofika Ukerewe kuanza kazi ya OCCID alikosa nyumba hivyo alikuwa anaishi nyumba ya Wageni.

Inadaiwa asubuhi ya leo walishangaa mtu haamki, walivyo bomoa Mlango wakakuta Kapoteza Maisha.

Kuhusu sababu za kifo chake tusubiri Mamlaka husika zitaelezea.

Masoud atazikwa kesho saa kumi pale Tabora mjini maeneo ya Kiloleni ya Ghana karibu ya tanesco ya zamani

Hivi karibuni Masoud Mohammed video yake ilisambaa mitandaoni akighani Qur'an Tukufu vizuri sana. Angalia Video yake hapa chini

Mei 09, 2020:

Azikwa rasmi

3BE5572E-3E37-43F0-9763-353696213493.jpeg

Kamanda wa Polisi Wilaya ya Ukerewe Masoud Mohamed amefariki dunia ghafla akiwa ndani ya hoteli.

Afande Masoud alijizolea umaarufu katika mitandao ya kijamii kwa usomaji wa Quran.

Taarifa zaidi kutoka Jeshi la Polisi zitakujia.

View attachment 1443731

Hawapendi kusikia vifo vimeongezeka. Acha tuwasaidie:

Ama kweli vifo vimepungua sana siku hizi.
 
Kamanda wa Polisi Wilaya ya Ukerewe Masoud Mohamed amefariki dunia ghafla akiwa ndani ya hoteli.

Afande Masoud alijizolea umaarufu katika mitandao ya kijamii kwa usomaji wa Quran.

Taarifa zaidi kutoka Jeshi la Polisi zitakujia.

View attachment 1443731
Juzi tuu nilimpost humu nikashauri bora aendelee kuwa imamu ona sasa kahamia kwenye mbao.
R.i.p kamanda.
 
Back
Top Bottom