TANZIA Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Ukerewe, Masoud Mohamed akutwa hotelini akiwa ameaga dunia

TANZIA Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Ukerewe, Masoud Mohamed akutwa hotelini akiwa ameaga dunia

Kamanda wa Polisi Wilaya ya Ukerewe Masoud Mohamed amefariki dunia ghafla akiwa ndani ya hoteli.

Afande Masoud alijizolea umaarufu katika mitandao ya kijamii kwa usomaji wa Quran.

Taarifa zaidi kutoka Jeshi la Polisi zitakujia.

View attachment 1443731
Mungu ailaze pahali pema roho ya marehemu.Amen.
 
Kamanda wa Polisi Wilaya ya Ukerewe Masoud Mohamed amefariki dunia ghafla akiwa ndani ya hoteli.

Afande Masoud alijizolea umaarufu katika mitandao ya kijamii kwa usomaji wa Quran.

Taarifa zaidi kutoka Jeshi la Polisi zitakujia.

View attachment 1443731

Rekebisha sio kamanda wa polisi wilaya ya ukerewe ni
OC CID / Kachero mkuu wilaya ya ukerewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daah! Poleni wana Kaloleni Tabora kwa kufiwa na huyu kamanda Masoud

5/5
 
Salaam wakuu,
IMG_20200508_162137_484.jpg

OCCID wa Wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza,Masoud Mohammed amekutwa kafariki sehemu aliyofikia.

Masoud Mohammed ni moja wa Maaskari waliobadilishwa Vituo hivi karibu.

Ukerewe ni kituo chake kipya cha kazi wakati kituo chake cha zamani cha kazi ni Bunda Mkoani Mara.

Masoud Mohammed ndo kwanza alikuwa kapandishwa Cheo cha kuwa OCCID hata hana muda mrefu na kituo chake cha kazi cha kufanya kazi kama OCCID ilikuwa ni hapo Ukerewe.

Alipofika Ukerewe kuanza kazi ya OCCID alikosa nyumba hivyo alikuwa anaishi nyumba ya Wageni.

Inadaiwa asubuhi ya leo walishangaa mtu haamki, walivyo bomoa Mlango wakakuta Kapoteza Maisha.

Kuhusu sababu za kifo chake tusubiri Mamla husika zitaelezea.

Hivi karibuni Masoud Mohammed video yake ilisambaa mitandaoni akighani Qur'an Tukufu vizuri sana. Angalia Video yake hapa chini
 
Back
Top Bottom