Salaam wakuu,
View attachment 1443761
OCCID wa Wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza,Masoud Mohammed amekutwa kafariki sehemu aliyofikia.
Masoud Mohammed ni moja wa Maaskari waliobadilishwa Vituo hivi karibu.
Ukerewe ni kituo chake kipya cha kazi wakati kituo chake cha zamani cha kazi ni Bunda Mkoani Mara.
Masoud Mohammed ndo kwanza alikuwa kapandishwa Cheo cha kuwa OCCID hata hana muda mrefu na kituo chake cha kazi cha kufanya kazi kama OCCID ilikuwa ni hapo Ukerewe.
Alipofika Ukerewe kuanza kazi ya OCCID alikosa nyumba hivyo alikuwa anaishi nyumba ya Wageni.
Inadaiwa asubuhi ya leo walishangaa mtu haamki, walivyo bomoa Mlango wakakuta Kapoteza Maisha.
Kuhusu sababu za kifo chake tusubiri Mamla husika zitaelezea.
Hivi karibuni Masoud Mohammed video yake ilisambaa mitandaoni akighani Qur'an Tukufu vizuri sana. Angalia Video yake hapa chini