Mkuu wa Vituo vya Udhibiti wa Magonjwa Afrika: Tunatumaini Tanzania itashirikiana nasi na kutoa takwimu mpya za COVID-19

Mkuu wa Vituo vya Udhibiti wa Magonjwa Afrika: Tunatumaini Tanzania itashirikiana nasi na kutoa takwimu mpya za COVID-19

Cannabis

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2014
Posts
11,557
Reaction score
33,535
2020-05-07T000000Z_785843128_RC2OJG9WEOUW_RTRMADP_3_HEALTH-CORONAVIRUS-TANZANIA-TESTS.jpeg

Mkuu wa Vituo vya Afrika vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Afrika anasema "tunaendelea kubaki na matumaini" kwamba Tanzania itashirikiana kwa kutoa takwimu zake za COVID-19 hata kama Rais wa nchi hiyo alishatangaza ushindi dhidi janga hilo.

John Nkengasong anasema "wanaelewa hali hatarishi na umuhimu" katika taifa hilo la Afrika Mashariki, ambalo halijatoa takwimu za maambukizi ya virusi vya corona tangu mwishoni mwa mwezi Aprili. Idadi ya kesi za Tanzania bado zimekwama kwenye idadi ya 509, wakati viongozi wa upinzaji wakisema kuwa kuna makumi ya maelfu.

Rais John Magufuli katika ibada ya kanisa Jumapili alitangaza kwamba "korona katika nchi yetu imeondolewa na nguvu za Mungu," na aliisifu waumini kwa kutokuvaa barakoa.

Ameonya kuwa barakoa ambazo hazijakubaliwa na serikali zinaweza kuwa na virusi hivyo.

===

The head of the Africa Centers for Disease Control and Prevention says “we continue to remain hopeful” that Tanzania will cooperate by sharing its COVID-19 data even as the country’s president declared victory over the pandemic.

John Nkengasong says “they understand exactly what is at stake” in the East African nation, which has not updated its virus data since late April. Tanzania’s number of cases remains frozen at 509, while opposition leaders have asserted there are actually tens of thousands.

President John Magufuli at a church service on Sunday declared that “corona in our country has been removed by the powers of God,” and he praised the congregation for not wearing face masks. He has warned that masks not approved by the government could be infected with the virus.


Source: Tanzania coronavirus: Africa CDC hopeful 'frozen' stats will be updated | Africanews
 
Wamesema Tanzania COVID 19 imekwisha.
 
Waendelee kuishi kwa matumaini huku sisi tupo busy na haka kanyimbo ka binti yetu Zuchu

 
Kwani tukitoa takwimu ndio mnazo dawa za kutibu corona??

Hata mimi sioni mantiki ya kukazania eti tutoe takwimu - takwimu wanazitakia nini wakati dawa na chanjo za kudhibiti ugonjwa wala hawana!!

Hapa wanacho lenga ni kutaka kuleta taharuki na kuzisema sema vibaya baadhi ya Mataifa na kuchukulia takwimu hizo kulazimisha kufanyia majaribio ya chanjo na dawa za makampuni makubwa yanayo tengeneza dawa na chanjo huko Merikani, njama hizo watashirikiana na WHO.
 
Idadi ya kesi za Tanzania bado zimekwama kwenye idadi ya 509, wakati viongozi wa upinzaji wakisema kuwa kuna makumi ya maelfu.
Wewe endelea kuwasikiliza wapinzani. Sisi tulishaacha kuwasikiliza toka waliposusia vikao vya bunge kwakisingizio kuwa wanaenda kujitenda kumbe wameenda mji wa Bashite kula bata.
 
Back
Top Bottom