Mkuu wa wilaya aingia darasani-afundisha hesabu za maumbo

Mkuu wa wilaya aingia darasani-afundisha hesabu za maumbo

Huyu mkuu wa wilaya chama cha walimu inabidi wamshitaki kwa mkaguzi mkuu wa shule wa kanda kwasababu hakuwa na lesson plan na teaching aids alizokuwa nazo pistol na risasi anahatarisha maisha ya wanafunzi!
 
Baada ya hapo anajilipa posho(mishahara ya miezi3 ya mwl) kwa masaa hayo tu.
 
mwacheni mkuu wa wilaya ajikumbushie hesabu za enzi zake.
 
Hii teknik ya DC ingelipa sana enzi za 70s. Wakati wa bugaluu, bumping, afro, etc.
 
vituko vya wakuu wa wilaya haviishi huko kagera mmoja kawaambia wanafunzi walioandamana kuwa atawaswaga maafisa elimu wakafundishe bila kuzingatia idadi ya shule na madarasa na ile ya maafisa. unakumbuka mmoja wao aliwahipiga bakora walimu?
 
Mrishogambo brother nikweli hyo? Umeingia kufundisha? Mimi nashauri kama vikosi vya uokoaji vinavyofanyaga kazi, sasa wabunge,ma dc, rc, deo,mawaziri, wawahishwe kwenyeshule wakapge lecture. Umoja wa mataifa nao ucheki uwezekano wa msaada wa walim had mgomo utakapomalizika
 
Chalii amenijuza kuwa Mkuu wa Wilaya Korogwe ameingia darasani kufundisha hesabu za kujumlisha darasa la saba na maumbo darasa la sita kufuatia mgomo wa walimu. Mkuu huyo aliingia kupiga nondo hizo katika shule ya msingi Mazoezi-Mbeza iliyopo katikati ya mji wa Korogwe.

Kupata Ukuu wa Mkoa ujue si mchezo! Lazima usanii uwe mwingi Msanii Mkuu akuone. Teh! Teh! Teh! Teh! Teh!
 
Nusu mara kimo mara kitako nimekosea au nimepatia?
 
Back
Top Bottom