Mkuu wa wilaya Iringa, Kheri James, atoa onyo kali kwa Walimu Wakuu kuhusu Klabu za Kupinga Rushwa Mashuleni

Mkuu wa wilaya Iringa, Kheri James, atoa onyo kali kwa Walimu Wakuu kuhusu Klabu za Kupinga Rushwa Mashuleni

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Kheri James, ametoa onyo kali kwa walimu wakuu wote wanaopinga uwepo wa klabu za kupinga rushwa mashuleni, akisisitiza kuwa serikali haitawavumilia wale watakaobainika kuhujumu juhudi hizo. Kauli hii aliitoa akiwa mgeni rasmi katika mahafali ya klabu za wapinga rushwa (PCCB CLUBs) yaliyofanyika tarehe 22 Machi 2025, katika Shule ya Wasichana Ifunda, mkoani Iringa.

Kheri James aliongeza kuwa mapambano dhidi ya rushwa ni jukumu la kila Mtanzania, bila kujali nafasi yake katika jamii kwani ni muhimu kwa vijana kupewa elimu ya kupinga rushwa tangu wakiwa shuleni ili waweze kuwa viongozi waadilifu.

“Kama kuna Mkuu wa shule ambaye hawezi kuwapa ushirikiano walezi wa hizi klabu, atafute shule ya kwenda sio lazima abaki kwenye shule hiyo” amesema Kheri

Maafali hayo yalikutanisha wanafunzi wa kidato cha sita kutoka shule mbalimbali zilizopo Wilaya ya Iringa, ikiwemo Shule ya Sekodnari ya Wasichana Iringa, Shule ya Sekondari Tosamaganga, Shule ya Sekondari Ifunda Tech, ambapo walipigwa msasa juu ya madhara ya rushwa na namna ya kupambana nayo.

Klabu za PCCB ziliundwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kama sehemu ya jitihada za kuhamasisha vijana kuwa mabalozi wa kupinga rushwa katika jamii zao.

 
Back
Top Bottom