LGE2024 Mkuu wa Wilaya Iringa: Mawakala wa Vyama vya Siasa wameridhika na zoezi la uandikishaji wapiga kura Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

LGE2024 Mkuu wa Wilaya Iringa: Mawakala wa Vyama vya Siasa wameridhika na zoezi la uandikishaji wapiga kura Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Bwana Kheri James amesema kote walikopita wilani humo mawakala wa vyama vya siasa hawakuwa na manung'uniko yoyote, wamerdhika kabisa na jinsi zoezi linavyoenda.

Sasa kule Chunga na Dar mnakwama wapi kufanya zoezi hili liende kistaarabu kama wenzenu wa Iringa?

=====

Ikiwa imebaki siku moja kutamatisha zoezi la uandikishaji wa wapiga kura katika daftari la makazi, Mkuu wa Wilaya ya Iringa Kheri James amesema kuwa mawakala wa Vyama vya siasa wameridhika na namna ambavyo zoezi hilo linavyokwenda kwenye vituo vyote vya kujiandikishia katika Wilaya yake.

DC Kheri James ameyasema hayo leo Oktoba 19, 2024 akiwa katika Kata ya Ruaha iliyopo Manispaa ya Iringa baada ya kuhitimisha ziara ya kutembelea vituo vya kuandikisha wapiga kura katika Kata za Ruaha, Kitwiru, Kihesa na Nduli ili kutambua mwamko wa wananchi kujitokeza katika siku za mwisho za zoezi la kujiandikisha kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa.

Kupata matukio yote ya mkoa huu soma: Yanayojiri kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mkoa wa Iringa

Aidha, DC Kheri James ameongeza kuwa, Vyama vya kisiasa vikiridhika na zoezi hilo, hiyo ni hatua ya kwanza ya mafanikio kuelekea kwenye mchakato wa uchaguzi kwa kuwa vyama vya siasa ni wadau wa msingi katika uchaguzi wa Serikali za mitaa.

Sambamba na hayo, DC Kheri James ameendelea kuwakumbusha wananchi ambao bado hawajajiandikisha kufanya hivyo kwa kuwa muda bado upo mpaka kufika kesho jioni.


Pia soma:
LGE2024 - Uzi Maalum wa Kasoro na Rafu kwenye zoezi zima la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
 
Back
Top Bottom