Mkuu wa Wilaya Jokate akutana na wabunge wa Korogwe mjini na vijijini kujadili mikakati ya wilaya ya Korogwe

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe mhe.Jokate Mwegelo mapema Leo hii April 17,2023 amekutana na Mbunge wa Korogwe mjini Dr. Alfred Kimea na Korogwe vijijini Timotheo Mzava ofisini kwake.

Katika Mazungumzo ambayo yamefanyika kwa muda wa saa Moja wabunge pamoja na mkuu wa Wilaya wamejadili mikakati ya Wilaya ya Korogwe pamoja na Changamoto zinazowakabiri wananchi wa Korogwe na namna ya kutatua Changamoto hizo Ili wananchi waweze kufaidi matunda ya Serikali Yao.

Pia wamezungumza kwa habari ya kudumisha/kuendeleza ushirikiano kati ya ofisi ya Mkuu wa Wilaya na ofisi za wabunge wa majimbo yote mawili.

 
Mtu huwezi amini mji wa Korogwe ulikuwepo tangu enzi ya Mjerumani, kila kitu kimekufa.

Magu kawajengea stand mpya lakini wenye mabasi wanaingia kwa kulazimishwa kwa dk zisizo zidi tano.

DC atafute wa kumshauri nyanja za kuinua vipato vya majimbo yote mawili sio wabunge ambao kuanzia yule "profesa" mganga wa kienyeji hawana mchango wowote wa maana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…