Hivi mlishawahi kuhoji juu ya wale wabunge wa viti maalumu wa chadema wenye undugu na viongozi wa juu wa chadema au mnayaona ya ccm tu?Ccm ni ile ile hata aje nani kwa mfumo wa ccm ulivyo nikazi bure
Sasa kwa Elimu aliyo nayo hawezi kuwa mkuu wa wilaya?aliipata kwa elimu aliyokuwa nayo
Hata mimi namuendeleza mwanangu, nikipata urais tu lazima apate ukuu wa uteuzi. Huwa tunamchagua mmoja tu katika familia. Chukulia Enzi za Mwinyi, Mkapa alimwendeleza wake kwa style tofauti kidogo, njoo awamu ya Kikwete (Ridhwan), sasa Magu naye sawaa....Kama anajitosheleza mwache awe...
kwenye uzi wake umeona wapi aliposema hana sifa?au alipopinga uteuzi wake?Kwahio kama amemlea na anazo sifa za kuteuliwa basi aachwe?
Well said, kwakweli katiba mpya iletwe na kada zote za viongozi labda iachwe Ukuu wa mikoa tu watu waaply kwavigezomvitakavyowekwa na wanaotakawaaply hii itaondosha mashaka!Wewe unaelewa maana ya conflict of interest au unaleta ushabiki maandazi hapa. Huyo mteuliwa kwa misingi ya undugu anaweza akatumia madaraka vibaya kwa kuwadhulumu watu au kuwanyima haki kwa vile ameteuliwa kwa misingi ya nepotism. Hata kama anazo sifa, hakutakiwa kumpa nafasi kama ya ukuu wa wilaya ambayo ina uhusiano wa moja kwa moja na kazi ya "Baba" yake. Je atawatendea haki wapinzani wa "baba" yake? Je mkuu wa mkoa atakuwa na uhuru wa kumuwajibisha "mtoto wa raisi"?
Kama hii habari ni ya ukweli basi tukubaliane kuwa misingi ya utawala bora imekiukwa na ifikie wakati haya mambo yawepo kwenye katiba ya nchi.

Hapa tunajadiliana na watu ambao hawana hata ABC ya uongozi. Ni watu waliojaa mahaba na mapenzi kwa chama. Ninyi hamna msaada kwa Taifa.
Watu wamebaki kwa kusema mbona utawala uliopita ulimweka fulani na fulani, wanachoshindwa kujua ni kuwa binadamu yeyote mwenye akili hatafuti kushindanishwa katika uovu. Halafu kuna hoja za kijinga kabisa kuwa mbona Ridhiwani alikuwa mbunge. Lakini Ridhiwani hakupewa ubunge na Baba yake bali alichaguliwa na wananchi. Huyo dada angekuwa amepata nafasi kwa kuchaguliwa na wananchi, kusingekuwa na hoja. Kama huyo binti angekuwa kwenye nafasi ya kitaalam kusingekuwa na shida. Lakini yeye amepewa nafasi ya kisiasa na mtu mwenye maslahi naye, ambaye kwa vyovyote vile au uteuzi wake, au mwenendo wake, au hatua dhidi yake au maumuzi yoyote dhidi yake, yanaweza kuathiriwa na mahusiano ya kifamilia.
Kama ni kweli haya yanayotamkwa, basi huyu atakuwa ndiye kiongozi wa kwanza Tanzania kumteua mwanafamilia kwenye nafasi ya kisiasa.
Kuwa kiongozi ni kujitoa, ni kuwa sadaka. Ukitaka kuwa kiongozi ujue kuna mambo utayakosa na kuna ambayo utapata ambayo wengine hawapati. Hali kadhalika familia yako nzima. Bila ya kujali kama sifa anazo au hana, huu ni ukosefu mkubwa wa uadilifu katika uongozi. Lakini kwa sababu ni Afrika, yupo sahihi sana.
Happy amesoma na mdogo wangu wa kike UDOM....mimi huwa nadhani ni mwanae kabisa JPM,kumbe ni wa kumlea tu!!ana elimu nzuri japo sina hakika na uwezo wake wa kiungozi