Tetesi: Mkuu wa Wilaya Mpya wa Kisarawe ni "Mtoto" wa Rais Magufuli

Tetesi: Mkuu wa Wilaya Mpya wa Kisarawe ni "Mtoto" wa Rais Magufuli

Kama anajitosheleza mwache awe...
Hata mimi namuendeleza mwanangu, nikipata urais tu lazima apate ukuu wa uteuzi. Huwa tunamchagua mmoja tu katika familia. Chukulia Enzi za Mwinyi, Mkapa alimwendeleza wake kwa style tofauti kidogo, njoo awamu ya Kikwete (Ridhwan), sasa Magu naye sawaa....
Kuna mtu hapo juu kasema Ridhwani akuteuliwa bali alichaguliwa na wananchi kuwa mbunge, wapiii.... unafikili bila mzee angeteuliwa na ccm kugombea!
 
Wewe unaelewa maana ya conflict of interest au unaleta ushabiki maandazi hapa. Huyo mteuliwa kwa misingi ya undugu anaweza akatumia madaraka vibaya kwa kuwadhulumu watu au kuwanyima haki kwa vile ameteuliwa kwa misingi ya nepotism. Hata kama anazo sifa, hakutakiwa kumpa nafasi kama ya ukuu wa wilaya ambayo ina uhusiano wa moja kwa moja na kazi ya "Baba" yake. Je atawatendea haki wapinzani wa "baba" yake? Je mkuu wa mkoa atakuwa na uhuru wa kumuwajibisha "mtoto wa raisi"?

Kama hii habari ni ya ukweli basi tukubaliane kuwa misingi ya utawala bora imekiukwa na ifikie wakati haya mambo yawepo kwenye katiba ya nchi.
Well said, kwakweli katiba mpya iletwe na kada zote za viongozi labda iachwe Ukuu wa mikoa tu watu waaply kwavigezomvitakavyowekwa na wanaotakawaaply hii itaondosha mashaka!
 
Wewe unaelewa maana ya conflict of interest au unaleta ushabiki maandazi hapa. Huyo mteuliwa kwa misingi ya undugu anaweza akatumia madaraka vibaya kwa kuwadhulumu watu au kuwanyima haki kwa vile ameteuliwa kwa misingi ya nepotism. Hata kama anazo sifa, hakutakiwa kumpa nafasi kama ya ukuu wa wilaya ambayo ina uhusiano wa moja kwa moja na kazi ya "Baba" yake. Je atawatendea haki wapinzani wa "baba" yake? Je mkuu wa mkoa atakuwa na uhuru wa kumuwajibisha "mtoto wa raisi"?

Kama hii habari ni ya ukweli basi tukubaliane kuwa misingi ya utawala bora imekiukwa na ifikie wakati haya mambo yawepo kwenye katiba ya nchi.
Well said, kwakweli katiba mpya iletwe na kada zote za viongozi labda iachwe Ukuu wa mikoa tu watu waaply kwavigezomvitakavyowekwa na wanaotakawaaply hii itaondosha mashaka!
 
Mkwere
Unampa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Hongera ya nini kwani kuteuliwa inahitaji jitihada au ni kufahamiana tu na mamlaka ya Uteuzi. Hakuna interview it's only at the Pleasure of the President. Tuache unazi of course miaka yote Marais wa Tanzania wamekuwa na a very high degree ya kuchagua ndugu zao na hata watoto ila awamu hii imezidi na ukanda ndio usiseme. Mbegu wanayochekelea CCM utakuja kuwa laana kwa Taifa la Kesho
 
Hata angekuwa mtoto wake wa kuzaa,Mimi sioni tatizo so long As Ana merits za kuwa mkuu wa wilaya.
Hata hivyo,kamuharibia angemuacha afanye kazi za kitaaluma,instead of hizi siasa za u dc na uchama
 
Hapa tunajadiliana na watu ambao hawana hata ABC ya uongozi. Ni watu waliojaa mahaba na mapenzi kwa chama. Ninyi hamna msaada kwa Taifa.

Watu wamebaki kwa kusema mbona utawala uliopita ulimweka fulani na fulani, wanachoshindwa kujua ni kuwa binadamu yeyote mwenye akili hatafuti kushindanishwa katika uovu. Halafu kuna hoja za kijinga kabisa kuwa mbona Ridhiwani alikuwa mbunge. Lakini Ridhiwani hakupewa ubunge na Baba yake bali alichaguliwa na wananchi. Huyo dada angekuwa amepata nafasi kwa kuchaguliwa na wananchi, kusingekuwa na hoja. Kama huyo binti angekuwa kwenye nafasi ya kitaalam kusingekuwa na shida. Lakini yeye amepewa nafasi ya kisiasa na mtu mwenye maslahi naye, ambaye kwa vyovyote vile au uteuzi wake, au mwenendo wake, au hatua dhidi yake au maumuzi yoyote dhidi yake, yanaweza kuathiriwa na mahusiano ya kifamilia.

Kama ni kweli haya yanayotamkwa, basi huyu atakuwa ndiye kiongozi wa kwanza Tanzania kumteua mwanafamilia kwenye nafasi ya kisiasa.

Mkuu hapo nilipoweka nyekundu sina hakika kama ulikuwa na maana ya "wao" ukaandinka "ninyi"!

Kama hukukosea ina maana unaniunganisha na mimi kwenye hilo kundi ulilotaja wakati hoja yangu na yako hazina tofauti!
 
Kuwa kiongozi ni kujitoa, ni kuwa sadaka. Ukitaka kuwa kiongozi ujue kuna mambo utayakosa na kuna ambayo utapata ambayo wengine hawapati. Hali kadhalika familia yako nzima. Bila ya kujali kama sifa anazo au hana, huu ni ukosefu mkubwa wa uadilifu katika uongozi. Lakini kwa sababu ni Afrika, yupo sahihi sana.

Hiyo ni kanuni ya wapi!! Kwamba kuwa mtoto wa Kiongozi ni Kama laana...!!!! The Kenedys America unawafahamu? Swala ni uwezo na kuwa na Sifa stahiki..... Acha kupotosha hapa.....
 
mbona hata ww ungefanya hivyo, kuwa rais hakumwondolei mtu sifa zingine. .....naamini hajakosea na kama amemlea atakuwa anamfahamu sna na anajua anafaa kwa nafasi hiyo. ....kila la kheri wateule wote fanyeni kazi
 
Tuwe wakweli Afrika familia zetu ni extended families. Rais hawezi kuteuwa watu kutoka mbinguni au kuzimu lazima watoke kwenye jamii yetu. Asipokuwa mwanae atakuwa binamu, mjomba, shangazi, mpwa n.k
 
Kimsingi, binafsi sioni tatizo hapo...if and only if uteuzi huo haukusukumwa in any way na uhusiano wao but utendaji wake as a person.

Ingawa natambua ugumu wa kuchora mstari kati ya hayo mambo mawili pasi na kuacha shaka machoni mwa watu.

Hata hivyo, if it were mimi, nisingemteua ili kuepusha mijadala isio na lazima juu ya possibility ya conflict of interests. Watu wana haki ya kuhoji japo huwezi kumridhisha kila mtu.
 
Happy amesoma na mdogo wangu wa kike UDOM....mimi huwa nadhani ni mwanae kabisa JPM,kumbe ni wa kumlea tu!!ana elimu nzuri japo sina hakika na uwezo wake wa kiungozi

Kumbe ni wajuzi juzi tu Kwa maana ya udom??? Halafu amewahi kuwa hr manager tanroad mkoa wa tanga ( kwa maana ya bosi wa mahr) ni vizuri ukamuhoji nduguyo je kuna class mate wake mwingine aliyefikia vyeo hivyo?? au mafanikio hayo? naomba ulete mlejesho halafu tuanzie hapo.. may be she is extra genious than all her classmates...
 
Sio vibaya kama anauwezo wa kutosha wa kufanya kazi mengine yatakuwa ni majungu tu.
 
Back
Top Bottom