Sisi tunaangalia theme ya andiko. Lengo la andiko ni kumchafua mtu.Mkuu kwani jamaa kasema DC hafai?mim mwenyewe nampata sana huyu Dada....ntafunguka kesho
Mi sioni kosa la mleta mada...mbona andiko liko positive tu...wasiwasi wa watu ni nini??Huyo dada kashakuwa public figure,ngumu kuzuia kujadiliwa...Sioni cha ajabu hapo. Huyo aonyeshe uwezo wake kwenye nafasi yake,upeo wa elimu anao. Jamaa wa Ufipa wanachoshangaa ni kuwa siyo `baby` wa mshua.
Kabla hatujamwangalia Happy tuanze na Rose Kamili, Atropia, Ruth Mollel ............
Exactly mkuu, cha muhimu awe na uwezo tuHata sioni tatizo kama sifa anazo
Wewe unaelewa maana ya conflict of interest au unaleta ushabiki maandazi hapa. Huyo mteuliwa kwa misingi ya undugu anaweza akatumia madaraka vibaya kwa kuwadhulumu watu au kuwanyima haki kwa vile ameteuliwa kwa misingi ya nepotism. Hata kama anazo sifa, hakutakiwa kumpa nafasi kama ya ukuu wa wilaya ambayo ina uhusiano wa moja kwa moja na kazi ya "Baba" yake. Je atawatendea haki wapinzani wa "baba" yake? Je mkuu wa mkoa atakuwa na uhuru wa kumuwajibisha "mtoto wa raisi"?Isitoshe sio baba yake wa kumzaa shida iko wapi hapo?. Tatizo tunalolikataa wananchi ni kubeba mtu asiyebebeka...huyo dada anayo elimu nzuri tu...
Wangejua kuwa kila mtu anaagizwa akalete wake wala wasingelalamikaToa data watu watachangia hakuna haja ya kuporomosha matusi. Katiba yetu inamruhusu raisi kufanya uchaguzi wake na vile hatuna wakuwathibitisha hawa (cf mawaziri) basi lolote laweza kutokea na upendeleo hapa si kitu cha ajabu kwani ikimpendeza mkuu unaweza kuchaguliwa. "You serve at the pleasure of the president". Kwa katiba hii inabidi tutegemee busara za raisi full stop.
Mkuu, ukuu wa wilaya hauombwi, ni cheo cha kuteuliwa.Usigeuze JF kuwa chungu cha majungu! Ongelea uwezo wake, sio uhusiano wake...ungejisikiaje kama ungekuwa wewe unaomba kazi sehemu afu unanyimwa simply because wewe una undugu na rais...tuletee CV na track record ya performance sio mijungu
Mkuu umefafanua vizuri. Nataraji wachangiaji watasoma comment yako.Wewe unaelewa maana ya conflict of interest au unaleta ushabiki maandazi hapa. Huyo mteuliwa kwa misingi ya undugu anaweza akatumia madaraka vibaya kwa kuwadhulumu watu au kuwanyima haki kwa vile ameteuliwa kwa misingi ya nepotism. Hata kama anazo sifa, hakutakiwa kumpa nafasi kama ya ukuu wa wilaya ambayo ina uhusiano wa moja kwa moja na kazi ya "Baba" yake. Je atawatendea haki wapinzani wa "baba" yake? Je mkuu wa mkoa atakuwa na uhuru wa kumuwajibisha "mtoto wa raisi"?
Kama hii habari ni ya ukweli basi tukubaliane kuwa misingi ya utawala bora imekiukwa na ifikie wakati haya mambo yawepo kwenye katiba ya nchi.