Poor arguement. Conflict of interest haiangalii sifa ya mhusika huangalia tu mazingira yaani kuna mazingira ambayo yanaweza kuwa yametoa upendeleo kutokana na mhusika kuwa na maslahi na mhusika.
Sifa ulizozitaja inawezekana kweli anazo lakini je hizo sifa ni yeye tu aliye nazo? Hakuna wengine walio na sifa kama yeye au kumzidi. Ni nini kilichomtofautisha yeye na hao wengine? Kwa kuwa hatujui, ndiyo maana kimaadili haitarajiwi kumpa kitu chochote chenye manufaa mtu ambaye wewe una maslhai naye kwa kupitia nafasi uliyopewa na umma. Hapa uteuzi huu unafanana kabisa na angalizo alilolitoa Mwalimu kuhusiana na corruption. Mwalimu alisema, 'corruption ipo katika mataifa mengi lakini mbaya zaidi ipo Africa. Asia mtoto wa Rais au mjomba wake atapewa tenda ya kutengeneza barabara, na barabara itatengenezwa, tena kwa viwango sahihi. Corruption ya Africa, tenda ya barabara atapewa mtoto au mjomba wa Rais, hela italipwa na barabara hamtaiona, lakini zote ni corruption.' Kama huyu mteule ana uwezo na sifa, kazi itafanyika lakini haitafuta ukweli kuwa kuna ukosefu wa maadili.
First, I don't see any competing professional or personal interest that can make it difficult for Magufuli to fulfill his duties impartially. PERIOD. Pili, uhusiano wa JPM na Happy ni tetesi tu there is no factual or empirical evidences to support this claim. Baloney.