Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Serikali imetoa ufafanuzi juu ya Wananchi wa Tambukareli, Kata ya Nsololo, Wilaya ya Uyui ambao wanadai malipo baada ya kutakiwa kuondoa kupisha mradi wa Reli ya Kisasa ya SGR.
Awali baadhi ya Wananchi hao walikaa kikao na kuiomba Serikali kutoa ufafanuzi juu ya malipo yao ya fidia kupisha ujenzi wa Mradi wa Reli ya Kisasa ya SGR, wakidai licha ya kufanyiwa tathimini tangu Machi 2023, hawajapokea malipo hadi sasa Mei 2024 na hawajui hatima ya malipo yao.
Zaidi kuhusu malalamiko yao soma hapa - Tabora – Uyui: Wananchi waliotakiwa kupisha Mradi wa SGR waomba Serikali isaidie walipwe fidia zao
Ufafanuzi wa Mkuu wa Wilaya
Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora, Zacharia Mwansasu alipotafutwa na JamiiForums amesema:
Inatakiwa ijulikane hawajalipwa kwa sababu gani? Mchakato wa tathimini una taratibu zake, mfano inaweza kutokea aliyefanyiwa tathimini akafariki au cheki ya malipo inaweza kuja kisha ikabainika kuna nyaraka zimekosekana, hivyo malipo yakakawama.
Ni haki la kila Mwananchi kuwasilisha malalamiko yake kwa Serikali, pia inatakiwa ijulikane ni fidia ya kitu gani, jengo? Nyumba? Kiwanja, Miti? Wanaodai ni wangapi? Na mamno mengine ya aina hiyo.
Wanachi wanatakiwa kufika ofisini kuwasilisha malalamiko yao, huu ni mradi wenye gharama kubwa, umetokea Dar es Salaam, imewahi kutokea malalamiko ya Wananchi wakalalamika huko kwingine, kwanini iwe Uyui pekee?
Namba yangu wanayo, nimeshafanya mikutano ya hadhara mingi tu nikishirikisha hadi TRC, namba yangu wanayo, maelezo yote nimeshawafikishia.
Ukihitaji Ushahidi zaidi njoo ofisini ili uone Ushahidi na uunganishe na hicho walicholalamika Wananchi.