Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Amshusha kwenye Gari Mwandishi wa Habari wa Wapo Radio

Huu ni uandishi wa Mwandishi?
 
Kwani U-DC unasomewa. Si kila DC ni anavyoona yeye? Anasahau kuwa gari anayotumia si gari binafsi na yeye pale ni mwakilishi wa Rais wetu na mwandishi ni mwananchi. Hatakiwi kudhalilishwa kwa namna yo yote ile kama ambavyo yeye DC pia hatakiwi kudhalilishwa kwa namna yo yote ile.
 
Hiyo ndio CCM, baada ya kuwatia mfukoni.
 
Mwandishi huyu kumbe anaandika story wakati mkuu wa wilaya anataka kwenda na waandishi wa HABARI.
 
Waandishi mngekuwa na umoja wote mngeshuka. ila hamna umoja, mwenzenu anashushwa nyie mnaendelea kuandika habari za huyu DC!
 
Usitetee rushwa, mnapenda sana rushwa! Ukipanda gari lake lazima utaandika kumsifia yeye na Wapo Radio hizo ndiyo zenu. Wapo Radio nyie hujifanya kuwa ni ya chama cha mapinduzi wakati siyo! Jitegemee kwa usafiri ili uandike habari zisizo a kujikomba.
 
Kwanini uombe lifti?

Mwambieni Boss wenu awanunulie magari ama awape posho kwa ajili ya kukodi magari kwenye kazi zenu.

Wako,

Kitimoto Kitamu
Kama hujui taratibu za watu kufanya kazi bora kukaa kimya tu, misafara yote ya viongozi huwa kila chombo cha habari kinakuwa na usafiri wake?ina maana lile gari ambalo idara ya mawasiliano ikulu , na wizara nyingine huwa linaandaa kwa ajili ya waandishi huwa hawaelewi?mtu unajipendekeza hadi boss ana ona kero!!!
 
Kama ndoa wewe mwandishi basi DC anywe bia popote pale alipo .

Kwa uandishi huu hata ungeenda kuandika ungeandika uchafu tu,

Kwanza tangu lini mwandishi akapewa lifiti na mtu anayetaka kwenda kuandika habari zake?

Si ungeegemea upande wake?


Wewe huna tja yoyote.Bora ulivyoshushwa ungeenda kumpamba tu.
 
Hapo ndio rushwa inaanzia hakuna sheria inaruhusu ujinga huo. Ni serikali yenu ya Julius ndio imekuwa na tabia za kichawi. Kosa kubwa sana kupanda gari ya taasisi unayoenda kucover story. Citizen ya Kenya wanajitegemea kwa kila kitu. Hata wewe ambaye umeleta hii habari sio mwanataaluma wa habari. Media house nyingi Tanzania zimewekwa mifukoni na DED, DC, RC na Directors wa mashirika. Kuweni huru andikeni habari bila kubase sehemu yoyote. Huyu DC inabidi apewe joto la jiwe. Nimekuwa karibu na International media wapo huru sana, hauwezi kusikia CNN wanakuja nchini wanapokelewa na migari ya STG.
 
Kama wewe ndio mwandishi uliyeshushwa na huu ndio uandishi wako.

Basi DC katufanyia wepesi sana, TUSINGEKUELEWA
Mwandishi kilaza, DC alifanya vizuri kumshusha! Hivi vyombo vya habari vya siku sijui wanatoa wapi hawa vilaza, kuna watoto flan wapo Mwanahls online, aisee wanapokuwa wanareport tukio aibu huwa naona mimi mtazamaji
 
Mkuu Josh J, kwanza asante kutuletea taarifa ya tukio hili.
  1. Sio kazi ya DC, or mtoa habari yoyote kuwapatia waandishi wowote usafiri. Kazi ya chombo cha habari na waandishi wa habari ni kutafuta habari, kazi ya serikali na viongozi wake ni kutoa habari.
  2. Kufuatia umasikini mkubwa uliotopea unaoikabili sekta ya habari Tanzania, sio vyombo vyote vina usafiri na sio waandishi wote wana usafiri, hivyo mtu mwenye tukio lake ili liwe covered, itampasa kuwa facilitate waandishi ama kwa kuwapa physical transport au kuwapatia tule tu bahasha za usafiri. But this is a favour not a right. Waandishi wa Habari na Bahasha: Sio Kila Bahasha ni Rushwa - Pasco wa JF!
  3. Kwenye ziara za viongozi mikoani, RAS hutoa gari la media. This is favour kwa waandishi tuu walio alikwa, ikitokea mwandishi amejiunga msafara bila kualikwa, akibainika, anashushwa ili kuondoa uwajibikaji kwa chombo ambacho hakijaalikwa.
  4. Kufuatia umasikini uliotopea kwenye media, baadhi ya waandishi ambao hawakualikwa, hujialika kwenye misafara na wakati wa kugawana posho ya usafiri, wanalazimisha lazima na wao wapate, hivyo ili kuzuia tusionane wabaya mbele ya safari, bora kumshusha kabla ya kufika na kuachana nae.
  5. Mimi ni muumini wa uwezeshaji waandishi, na zile bahasha, mimi ndio msambaza.
  6. Siungi mkono kabisa tabia za waandishi kujialika kwenye closed events. Waandishi wako huru kuhudhuria all public events, lakini kwa closed events, ni lazima waalikwe. Kama hujaalikwa ni halali kufukuzwa au kushushwa njiani.
  7. Siungi mkono tabia ya waandishi kuvamia events za watu bila kualikwa na wakati wa lunchtime wao ndio wa kwanza na wanavyojaza hizo sahani misosi...
  8. Siungi mkono waandishi kwenye hafla za mchapalo, kufakamia vinywaji na within no time wanakuwa wako njwii!.
  9. Siungi mkono tabia ya waandishi kugombea posho kwenye events. Huku ni kujidhalilisha. Media, Tumedhalilishwa!, Tumejidhalilisha!. Ni Matokeo ya Sheria Mbovu, Umasikini, Dawa ni Kuunganisha Habari na UtangazajI, Tulipwe Fungu Nene!.
  10. Mwisho napigania usawa wa binadamu kwa waandishi, mkifanya tukio, mkalipana posho nene nene na nono nono, waandishi nao wawe treated the same. Sio mnahudhuria seminar, wenyewe mnalipana sitting allowances nene nene, waandishi mnawapa vibahasha vilivyo kondeana. Uhuru wa Habari Tanzania: Je, Vyombo Viko Huru? Je, Waandishi wa Habari wako huru? Wanathaminiwa?.
P
 
Kwa uandishi huu wewe ni kilaza na hustahili kutoa habari yo yote!
 
Kwa uandishi huu wewe ni kilaza na hustahili kutoa habari yo yote!
Acha kuwa Mpumbavu, Mbwa Wewe, Ni Wapi Nimeandika Kwamba Nimeandika Mimi Josh J? Mpumbavu Sana Ww
 
Acha kuwa Mpumbavu, Mbwa Wewe, Ni Wapi Nimeandika Kwamba Nimeandika Mimi Josh J? Mpumbavu Sana Ww
Duuh! Kumbe una upungufu wa akili kichwani, sasa tukusaidieje! Ungepungukiwa damu tungekusaidia!
 
Tena umekodiwa na Bodaboda shukuru Mungu maana wengine wangekuacha utembee kwa mguu, wandishi wa Wa bongo njaa kali sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…