Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Victoria Charles Mwanziva awasili Ludewa

Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Victoria Charles Mwanziva awasili Ludewa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Victoria Charles Mwanziva tarehe 30 Januari 2023 amewasili rasmi Ludewa.

WhatsApp Image 2023-01-31 at 15.03.06.jpeg

Victoria Charles Mwanziva alipokelewa kwa kishindo na Viongozi, Skauti wa Shule ya Sekondari Chief Kidulile na Wananchi mbalimbali wa Wilaya ya Ludewa.

Aidha, Mhe Victoria Charles Mwanziva amefika na kukabidhiwa Ofisi na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Andrea Tsere. Baada ya kukabidhiwa Ofisi, Victoria Charles Mwanziva alifanya kikao na kamati yake ya ulinzi na usalama ya Wilaya.

WhatsApp Image 2023-01-31 at 15.03.05(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-01-31 at 15.03.06(1).jpeg

Aidha, Victoria Charles Mwanziva aliwasili katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kukutana na viongozi mbalimbali wa CCM na Idara zake (UWT, UVCCM na Wazazi) wa Wilaya ya Ludewa.

"Ludewa ya Utalii. Uchumi wa Chuma kwa Maendeleo Yetu."

WhatsApp Image 2023-01-31 at 15.03.07.jpeg
WhatsApp Image 2023-01-31 at 15.03.05.jpeg

#LudewaYetu
#LudewaYaSamia
#UongoziShirikishi
#KaziIendelee
 
Mkuu, ziara yake ya kwanza mpelekeni kule Masmavalafu na Ibumi ambako hata network haikamati na hata zahanati ni shida. Sijui kama wameshajenga Zahanati kwa sasa. Aende huko ili aone uhalisia wa Wilaya anayoongoza.

Akitoka huko aende maeneo ya Mwambao hadi Manda. Tsere amejitahidi kwa kiwango chake hapo Ludewa maana watu wa hapo wagumu sana.

Namuona pia hapo Afisa Tarafa huyo ndugu mrefu mwenye kofia nyeusi. Yeye kila tukio huwa hakosi. Ha ha haa.
 
Kuapishwa jana tu na leo kashafika ofisi ya chama na kukutana na kamati yake ya ulinzi na usalama......akumbuke Wakinga sio watu wazuri,apunguze mbwembwe
 
Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Victoria Charles Mwanziva tarehe 30 Januari 2023 amewasili rasmi Ludewa...
Huyu chawa anapenda promo na anatia kichefuchefu!! Hana muda maana petty politics zimepita!! Tuendako nguvu yako ya hoja ndo itakubakiza kwenye siasa sio pambio na kujipendekeza kuliko pitiliza.
 
Kuapishwa jana tu na leo kashafika ofisi ya chama na kukutana na kamati yake ya ulinzi na usalama......akumbuke Wakinga sio watu wazuri,apunguze mbwembwe
Kule hakuna Wakinga. Ni Wamanda, Wakisi na Wapangwa.
 
Vyeo vya kupeana tu hivi. Havina tija yoyote ile kwa Wananchi.
 
Kuapishwa jana tu na leo kashafika ofisi ya chama na kukutana na kamati yake ya ulinzi na usalama......akumbuke Wakinga sio watu wazuri,apunguze mbwembwe
Soma vizuri uelewe yuko wapi, amepelekwa Ludewa siyo Njombe.
 
Arrogance is very clear and no doubts hafai kabisa huyu kuwa DC... Publicity and cheap popularity naona ndio anajitangaza hovyo, mtu wa kazi hafanyi hizi petty politics
 
Back
Top Bottom