MKUU wa wilaya ya Morogoro, Albert Msando amepata ajali maeneo ya Dakawa mkoani Morogoro baada ya gari aliyokuwa amepanda kugongana uso kwa uso na gari jingine dogo.
Ajali hiyo imetokea wakati mkuu huyo wa Wilaya akiwa kwenye msafara wa ziara ya waziri Mkuu uliokuwa unatoka Dakawa kuelekea Morogoro mjini leo Jumamosi, Agosti 14, 2021.