Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Dkt. Sophia Mfaume akiongea kwa uchungu katika msiba wa Askari Polisi waliopoteza maisha katika majibizano ya risasi na majambazi wilayani humo.
Dkt. Sophia amesisitiza juu ya umuhimu wa Jeshi la Polisi katika ulinzi wa raia na mali zao na kutoa pole kwa jeshi hilo, familia na wananchi wote huku akisisitiza kuwa uhalifu wa namna hiyo hauna nafasi wilayani hapo.