Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Aliwahi kulazwa Muhimbili miezi 4 iliyopita kwa presha akaruhusiwa.
Mauti imemkuta akiwa kalazwa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mtwara Ligula, akisumbuliwa na maradhi ya Moyo.
Mmanda aliteuliwa kuwa mkuu wa Wilaya ya Mtwara na rais Magufuli 19 Dec 2016 akichukua nafasi ya Dkt. Khatib M Kazungu ambaye alihamishiwa Wizara ya Fedha.
Wakili Msomi Mmanda aliyekua pia mjumbe wa Bunge la Katiba. Katika Bunge hilo, aliteuliwa na MWENYEKITI wa Muda wa vikao vya Bunge Maalumu la Katiba, Pandu Ameir Kificho, kama mmoja ya wajumbe 20 Watakaomshauri ili kuboresha utendaji.
2015 alitangaza nia ya kugombea Ubunge jimbo la Rombo kupitia CCM.
UPDATE
SERIKALI KUSIMAMIA MAZISHI YAKE
“Tumekubaliana na familia kwamba sisi Serikali ndiyo tutakaosimamia mazishi yake…na hakutakuwa na kusafirisha mwili…atazikwa hapa Mtwara…na hatazikwa na zaidi ya watu kumi,” Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa akielezea taratibu za mazishi ya liyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Evod Mmanda aliyefariki dunia Aprili 26, 2020 katika Hospitali ya Rufaa Ligula alipokuwa akipatiwa matibabu.