Wizara ya Ardhi
Govt Institution
- May 14, 2024
- 306
- 165
Mkuu wa Wilaya ya Musoma mkoani Mara, Juma Chikoka, amewahimiza wananchi wa Wilaya hiyo kujitokeza katika Kliniki ya Ardhi inayofanyika katika Viwanja vya Mara Sekondari, ili kupata elimu na huduma mbalimbali zinazohusiana na masuala ya ardhi.
Aidha, Chikoka amesema kuwa yeye binafsi atashiriki katika Kliniki hiyo kwa muda wa siku tatu, kuanzia Septemba 28, 2026, ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma na elimu kuhusu masuala ya ardhi kwa wakati.
Kliniki ya Ardhi ni jitihada ya Serikali ya kusogeza huduma za sekta ya ardhi karibu na wananchi, ambapo kwa sasa inafanyika katika mikoa yote ya Tanzania Bara.
Kliniki hiyo ilizinduliwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Leonard Akwilapo tarehe 25 Septemba 2026 Mkoani Mtwara na inatarajiwa kuhitimishwa tarehe 3 Oktoba 2026.
Karibu tukuhudumie