Mkwasa: Tatizo sio wachezaji tatizo uwanja ulikuwa na koki za maji

Mkwasa: Tatizo sio wachezaji tatizo uwanja ulikuwa na koki za maji

Mpeni muda tu kwani bado tuna matatizo makubwa katika ufungaji s
 
Kwa mara ya kwanza leo ndio nimesikia utetezi wa kitoto kuliko wowote niliowahi sikia. Hayo mazingaombwe waliofanza hao Waarabu ni ya kiwapi tena? Maji yanachemkia pale mlipokanyaga nyie tu. Wao wakikanyaga panakauka?
Round ya kwanza kwao kukavu kwenyu kumejaa maji, mlipogeuka, kule kwao kukajaa maji na kule mlipokuwa kukakauka. Si ndo mngeshinda kwani wao sasa wanachezea kwenye maji?? Hii haiingii akilini kabisa.
Mkwasa, sema ulizidiwa akili na tena ni mara yako ya kwanza kwa timu yako kukutana na timu kuubwa namna hii, Tutakuelewa tu kuwa ulienda kutimiza wajibu ila ulijua ungefungwa tuu
 
hapa dar walikosa magoli ya wazi matano,wangekuwa makini wangeshinda hapa tano sisi ni wabishi tu kuanzia uongozi wa tff ulio kaa kitapeli tapeli tu mpaka uongozi wa hizi timu mbili za simba na yanga..Naskia wamerudisha matumaini tena baada ya kusikia kassim majaliwa kawa waziri mkuu kwamba atasaidia soka la bongo kisa alisha cheza mpira...Siku tukiwa serious na maisha yetu tukaacha mizaha,utani ,ulaghai tukaanza kujitambua tutafika mbali..we angalia yanga ni timu nzee hapa tz inakaribia kumaliza karne lakini haijawahi kuwa na kitegauchumi chochote hata cha chupi kama walivyo fanya tmk wanaume,tunaishi kimiujiza ujiza tu
 
[h=2]koki za maji[/h]kwa hiyo mlichezea koki mkaloa

Mkwasa dhana ya kitoto kabisa sisi tumeuona mchezo kwenye luninga.Mechi ya kwanza baada ya kuona timu karibu yote yanga ukabalance kwa kufanya sub zisizo na tija gori zikarudi.mechi ya pili timu ilipotea kabisa waarabu walicheza kama wako kwenye mazoezi.KUBALI YAISHE UWEZO WAKO UMEISHIA PALE
 
Kwa iyo Algeria walikua wanatumia mitumbwi wakija upande wa stars ili kukwepa msala wa koki??😂😂😂 waungwana wakivuliwa nguo wanachutama sasa naona Mkwasa kasahau hili
 
Mueleweni kocha, ni kwamba wale jamaa walijiandaa kufanya fitna, wao wakavaa viatu vya kucheza kwenye mvua na sisi hatukujiandaa kwa hilo, goli 7 tumepigwa, hata Brazil alichapwa hizo7 na siku hiyo stars anafungwa kuna nchi ipigwa 10-0, mwacheni mkwassa afanye kazi yake, Tff waitafutie timu mechi nyingi za majaribio hasa nchi za magharibi.
 
Kwa hiyo walizishangaa au?kama ni kosa kisheria mbona Fifa hawajasema.

Au walishangaa koki na je zilipofunguliwa wachezaji wa Algeria walikuwa wanachezea hewa hewani? Mfa maji huyu.
 
Kocha wa Kilimanjaros stars amedai tatizo kubwa la timu yake kupoteza ni hujuma walizofanyiwa na Algeria moja wapo ni kuwepo kwa koki za maji uwanjani (pitch).

Walifanya michezo hii kwenye upande stars na kubadilisha tena koki kufuata upande wa stars kwenye second half.

Nini maoni yako mwana michezo mwenzangu?

Hata kama zilikiwepo, ina maana hakukua na wasimamizi wa mechi akalalamika kwao?.
Kalio la baiskeli
 
Hata Brazil alipigwa hizo WC na Germany, tuwe wapole tu.
 
kuna jamaa aliniambia tumefungwa sababu golikipa wetu aliwekewa taa za disko kwenyegoli zikawa zinammulika, yaani analalamika mshabiki kipa kauchuna tu, mwambieni mkwasa mechi ilirushwa live asitudanganye kitu.
 
Mueleweni kocha, ni kwamba wale jamaa walijiandaa kufanya fitna, wao wakavaa viatu vya kucheza kwenye mvua na sisi hatukujiandaa kwa hilo, goli 7 tumepigwa, hata Brazil alichapwa hizo7 na siku hiyo stars anafungwa kuna nchi ipigwa 10-0, mwacheni mkwassa afanye kazi yake, Tff waitafutie timu mechi nyingi za majaribio hasa nchi za magharibi.
ungeniambia kuwa goli saba ni kitu cha kawaida ningekuelewa, sasa unasema wenzetu walijiandaa na mechi ya brazil na ujerumani nani alifungulia koki?
 
Duh ngumu kuamini. Ila angesema Algeria walituzidi kimchezo, kimazingira na kiftina tungemwelewa.....timu bora kutolewa na timu dhaifu hutokea Mara chache, pia sie TZ kama tunajisifu kucheza vizuri game ya kwanza nyumbani, tukatumia nguvu na wachezaji wote mahiri, tukaenda Algeria na walewale, wakati Algeria walisoma mchezo wetu, waliporudi kwao wakatumia siraha zao za maangamizi.
Sisi pia tulitumia advantage ya nyumbani, tukajifurahisha kiasi chake!! Nao pia wametumia fursa ya nyumbani kujifurahisha, sasa yupi katumia vizuri?
 
si afadhali ya koki!pia kadai wimbo wa taifa umechangia.eti wimbo wetu ulikuwa hausikiki kama wa kwao
 
Nafuu koki wangepigwa maji ya washwasha tungekaa 70 goals
 
Hata arsenal alifanyiwa hivyo na barcelona fainali uefa!
 
Hahahah daaah hi kali. Cjawah ona utetezi kama huu. Kwani koki zkfunguliwa upande mmoja si wanaadhrika wote watakaocheza upande huo. Kwa mfano ni upande wa stars kpa na mabek wataadhrka na washambiliaji wa Aljeria nao wangeshndwa kufunga.
 
Back
Top Bottom