Mkwasi Rostam na Vodacom



Hili ni wazo zuri lakini kama kuna uwezekano wa kufahamu kiasi cha share zake ingekuwa vema kabla ya kuchukua hatua. Ila mgomo kwa vyombo vyake vya habari (magazeti ya Rai, Mwanchi n.k.) ni vema ukaanza mara moja pamoja na biashara zake nyingine. Hii isiishie kwa Rostam tu, bali iendelee kwa biashara za wengineo zinazofahamika.
 


And guess who owns Caspian?
By the way hawa Caspian si ndio wanaojenga migodi ya Barick?
 
Mimi ninaona sio tu za RA, bali bishara nyingi za Mafisadi, hata ikiwa Bar. Nchi za wenzetu wanaangalia hayo mambo kwa njia tofauti kama Kampuni ina husika vipi katika kuharibu au uhifadhi wa Environment, Kuangalia wafanyakazi wake etc etc.
Sasa mkisusia hizo bidha zake , hao wengine wanaweza kuwafukuza, au kununua share zao, hivyo kuwagusa EL, na RA kwa hapo VODA, na hata hayo magazeti yake.
Na kwa wenye Hotel za Kitalii , kama ni mafisadi, pia tunaweza kuwaarifu wateja wao.
Huu ni mwanzo mzuri.
Nakumbuka Mbeya Cement na Issue ya Mgodi wa Kiwira kama ilikuwa kweli, kwamba Mbeya cement walikata kununua umeme wa Kiwira.
 
Miye nadhani anayeadhibiwa siye...! aliyeionyonya Tanzania na kuifikisha hapa siyo Rostam.
 
Sema wewe kiazi.....


Naamini Rostam ni chagua jepesi la kuadhibu; Ni sawasawa na mtu kumchagua ndama kwa mlo kwa sababu kashindwa kumkamata fahari. Rostam ana matatizo yake lakini yeye kama ndama anavyomuandama mama yake ili anyonye ndivyo yeye afanyavyo. Kumuadhibu yeye kwa kumng'ang'ania mama yake yawezekana tukawa tunalenga kusiko. Binafsi ningemshughulikia ng'ombe mwenyewe...
 

Who is ....... Mzee mbona umetuacha kwenye suspense hapo?
 

Mkuu MJJ,
Kumng'ang'ania RA sio vibaya maana ametumika sana katika kumuweka JK madarakani, kwa hiyo yeye sio ndama ni baberu kabisa. Kama Vodacom wata-bamizwa na kulazimishwa kumtema RA, wawekezaji wengine watafyata kuungana na mafisadi kwenye miradi yao nchini. Next labda itakuwa dala dala za Lowasa n.k. Hii inaweza ikasaidia kuibua mengine tusiyojua na pia kubadili hisia za watu juu ya mali za rushwa. Hivi sasa bado kuiibia nchi ni ujanja.
 

Mwanakijiji,
Kunapokuwa na panya wale wadogo nyumbani kwako wanaokula nguo, mama na mtoto wake,huwezi sema kuwa umwache mtoto kwanza kwa kuwahawezi kukimbia kama mama yake. Utakayekuwa na uwezo wa kumfikia ndo unaanza naye. Hapa bila shaka atakuwa mtoto kutokana na weakness yake ya kutimka kama mama. Ukishakaua katoto ndo unakusanya nguvu kumtafuta mama. hakuna wa kubaki. Lunyungu kasema wazi kuwa sio kuwa hao wengine tumewaacha, la hasha ila sio mbaya tukianza na huyu.

Unajua kwenye vita ni pamoja na kumshinda adui yako kirahisi bila ya kuwa na majeriuhi wengi kwa upande wako. Mbinu mojawapo wanayoitumia ni pamoja na kuhakikisha unakata njia zote za supply za adui.
 
Rostam ni matokeo tu na siyo chanzo.. chanzo kipo na hicho ndicho cha kukikata. Ninaelewa na ninakubali kuwa ipo haja ya kuwaadhibu watu ambao kuna ushahidi wa kuhusika kwao katika kulikomba Taifa letu. Lakini naamini lazima twende zaidi ya watu bali pia mifumo na vitu.
 
JF is where we dare to talk bila ya uoga.tafadhali tufungue macho wakati tuna hangaika na RA tuwe na mkakati wa huyo mwingine ila wote lazima tule nao tumesha choka kabisa kabisa
 


Maelezo ya Nyangumi hapo juu ni super, Mmwaa!

Ni kweli ni chaguo jepesi na ndio maana hata adhabu tumemchagulia nyepesi.
Kitakacho msibu ni aibu tu na pia atajifunza kutengeneza clean monies. What else do you think he will loose if he sell his shares, - nothing!

Tufanye jitihada ku-create awareness kuhusu possibilities tunazoweza kuchukua ili watu wengi zaidi watambue (binafsi wazo la Lunyungu halikuwemo kwenye fikra zangu). Tusilenge sana kwenye kuadhibu watu; that should not be our main focus.
After all nchi hii inaongozwa kwa sheria.

Please, msome tena Nyangumi.


.
 
naomba kujua maandalizi ama sms hizi zinatembea kweli ? Mbona sijapata moja kama mwana harakati kwamba tuachane na hawa jamaa ?
 
Nashauri tutumie line hizo hizo za Vodacom kupeleka message then unatupa na kuanza maisha mapaya tafadhali .
 
rostam anaweza kuwa si chanzo wala si mwisho wa ufisadi. na nia yetu ni kuufuta katika uso wa tanzania ufisadi, ila mtu hujikuna ajipatapo.
adhabu ndogo kwa rostam inaweza tu ikawa mfano kwa taifa kuwa watanzania sasa si watu wa kulalamika tu bali ni watu wa kuchukua hatua.
vinginevyo serikali kila siku itatupa ahadi bila matokeo
 
Miye nadhani anayeadhibiwa siye...! aliyeionyonya Tanzania na kuifikisha hapa siyo Rostam.

Mimi nakuunga mkono mzee mwenzangu, tatizo sisi watanzania kazi yetu ni kupenda kufuata mkumbo (yaani upepo unapoelekea na sisi huko huko) hatujua hata kupima uzito wa tunachoambiwa. Akitokea mtu akasema doma kaya fisadi basi watu wote wataanza kuniponda na kuniita fisadi bila hata ya kuwa na uhakika na wanachosema. Leo hii mtu mmoja anakuja na kusema tususie huduma ya VODA COM na watu karibu asilimia 90% wameunga mkono. Sishangai cos ndio watanzania tulivyo.
 
nani anajua celtel ni ya nani hapa?
atupe data kabla ya kuhamia huko, tigo na zantel pia. labda hizi kampuni mpya ndio kimbilio letu.
Manake navyojua mimi ya celtel yako jikoni, yanakuja, labda wana JF tuchoke na kushiba fisadi mmoja.
 
samahanini wenzangu kwa kuwakatisha stimu, lakini mimi naona hii agenda ni marketing strategy.
kila mtu anajua Rotam alikuwa na caspian kabla na baada ya vodacom, iweje voodacom ishambuliwe wakati caspian ipo?
mbona tunajidai wachambuzi lakini hakuna anaetaka kujua kiini cha Caspian yenyewe?
au kama rostam, au mojawapo ya kampuni tanzu zake anamiliki celtel au kampuni nyingine ya simu?
ina maana ukweli hautafutwi hapa?
siwezi kuamini hii data moja tu hapa ya share distribution ya vodacom ndio imelete mwamko mkubwa hivi wa watu 'kuhamia' celtel.
samahani tena
nahisi tunaendeleza 'hate' policies. Lengo liwe kuwa na nchi ambayo straight and transpatent policy zinafuatwa, sio kufuata upepo.
naomba kuwakilisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…