wakuu wangu wa hapa jamvini.
katika mapambano ni lazima kutofautiana, na katika kutofautiana kuna kuelimishana, baada ya watu kuelimishwa na kuonekana hawataki kuelimika, kama ni vitani kuna lazima au kuwaburuza mstari wa mbele. au kuwafungia ndani wasijue kinachoendelea. katika vita yetu dhidi ya ufisadi mkuu lunyungu ametupa somo murua. kuwa sasa tutumie silaha nyingine nyepesi nayo ni kususuia mafisadi kwa njia rahisi.
ni nani kati yenu atakayekataa kuwa rostam anatumia ulimbukeni wa wanasiasa wetu kujitajirisha kwa njia haramu na kwa hatari ya taifa letu.?
ni nani atabisha kuwa fisadi huyu ameshapitisha kile kiwango cha juu cha ile theory maarufu na sasa yuko pale juu kabisa anatafuta self actualization. kwa maana kwamba pesa zake hizo zifike mahali zimsadie ili awe hata mfalme wa nchi hii ili tusujudie na kumpgia magoti? pesa alizopata kwenye ufisadi.
ni nani kati yenu atakataa kuwa bila rostam na lowasa hakuna ccm? na ccm ni rostam na lowasa? na kuwa kikwete ni kama tarishi wao?
wakuu wangu kama tunaamini hayo tunayo silaha moja, silaha kama aliyotumia martin luther king, kwa kuwataka watu weusi wakasusuia mabasi ya watu weupe. na mwisho akafauku kuutokomeza ubaguzi wa rangi huko marekani kwa kiwangi kikubwa.
ni kweli kuwa tunao msururu wa kampuni za kifisadi, lakini kwa kuanznia tuanze na huyu na wengine watashtuka.
nitawaomba wakuu wengine hapa, katika ku-intesify vita hii, wanaofahamu wawaandkike pia vodafone uk, ambao wanamiliki pia vodacom kuwa vita imetangazwa, hii ni kuwaonya wanaojiita wawekezaji wanapokuja hapa nchini wawe macho na matapeli kama akina rostam
wanaosema eti tukisusia voda uchumi utaathirika wanaota ndoto za ajabu. wateja wa voda watahania mitandao mingine na huko serikali itaendelea kupata kodi yake. na wale waajiriwa wa voda itabidi wahamie kwenye kampuni nyingine za simu kwa kuwa ajira zitaongezeka sambamba na wateja wapyaa
WAKUU HAKUNA TUTAKACHOPOTEZA KATIKA HILI, BALI TUTAKUWA TUMEMPA FUNZO MAMVI NA HUYU MUAJEMI WAKE