Mkwe anapokuwa mke

Mkwe anapokuwa mke

Pole sana mamake..
Kweli itakuwa ngumu kumtenganisha
Mtu na mama yake sasa.. lakini binafsi
Naona kosa liko kwa mumeo. Kwa kutoongea
Nawe au kufanya vitu bila kukujulisha wewe
Mkeo..

Mkwe ye hupata kichwa
Sababu kijana yuko upande wake.
Kusema hivyo kuna sababu ambazo
Zinawafanya mama kung'ang'ania watoto
Wao wa kiume
Lakini hii ya kuingulia nyumba **** kiasi
Hiki imezidi..

Ushauri wangu washirikishe wazazi/walezi wako
Kwenye hili wenyewe wanajua zaidi cha
Kusema na kufanya
. Pole sana..

nakubaliana nawe AD. wazazi watajua namna nzuri ya kulimaliza hili bila ya bibie kujiingiza matatani sana na ma'mkwe wake!
 
hehehehe! kaa ngumu dada, huyo ni mumeo na hata mama mkwe afaa aelewe hayo. you are not there by mistake neither by chance and that you deserve total authority in any decision affecting your family. hata mumeo anafaa ajue kuwa wewe ndo mwenye boma na si vinginevyo na majukumu ya kumlea mama mkwe ni yako na si yeye hata kama ni mwanae. fungua macho mrembo na unoe kucha laa sivyo kesho kutwa utasikia mama kamshauri mwanae kuoa mke mwingine wewe hufai....chukua control haraka before it is too late. hata mimi mamangu alitaka kunicontrol jinsi nitaishi na mke wangu, nikashtuka mapema, nikakaa ngumu sasa ametii amri. heshima kwa mke wangu palepale
 
Wanajamvi kwa muda nimekuwa nikiumizwa na hili jambo. Mama mkwe wangu ni kama mke mwenzangu. Mume wangu anapanga budget na mama, kila kitu ni mama. juz kachukua mkopo bank nusu kampa mama afanye miradi. Nimejaribu kushare na familia mama kaja juu yeye ndio kamsomesha anastahil kuenziwa. Mume hashauriki bila kumshirikisha mamake. Hapa ana miez 6 tunakaa nae. Ni vurugu. Ushauri wandugu.
maskini halafu hali yako jinsi ilivyo tena....mh! si watakufupishia siku my dear????
 
pole sana, kaa na mumeo mueleze kwa kirefu ikibidi omba walio wazidi umri wamueleweshe.
 
Pole mpendwa hebu jaribu kuzungumza na mmeo kwa utaratibu yanayokukwaza na umwambie kabisa ahata bible inasema mwanamme ataachana na familia yake ,nae ataambatana na mkewe ,nao watakuwa mwili mmoja.. ambayo ni
Kupanga na kuamua pamoja
Maendeleo ya familia pamoja
NK NK
Huyu mama mkwe nae anatakiwa awe na hekima lol
imenisikitisha
 
nakulaumu kwa kukubali kuishi na mkwe, nijuavo mwanamke ndie kama waziri wa mambo ya ndani ktk nyumba, tell yo husbund achague moja kati yako ww au mama yake, umenikumbusha dada yangu nae alifanyiwa kama wewe, alimfungia kibwebwe na kuwasema wote akamuuliza mama mkwe wake kama anayomfanyia yeye nae alifanyiwa alipoolewa, akamwambia anaingilia ndoa yake na atamshtaki kwa padri akampaa saa 48 arudi kwao la sivo ataondoka yy na watoto. mume hakutii wala mama mkwe hakuondoka dada hakutania alichukua watoto wote akapanga nyumba pengine. mume alimrudisha mama yake akamchukua mke hadi leo wanaishi kwa amani na upendo.
kisa chako unakubali kuteseka sema na mwenzio mpe masharti asipokubali fanya maamuzi magumu ili uishi kwa amani kama kumpeleka kwa mchungaji na wazee wa kanisa weka wazi yote unayotendewa, kina dada wana tabia ya kuenga bila waume kujua ili yakitibuka kama haya wawe na pa kukimbilia nimeelewa sasa kwa nn wanafanya siri ktk kujenga,
wake up esperance usikubali kuumia take action b4 its too late,
 
Back
Top Bottom