Mlaani hapa kiongozi aliyekukosea

Mlaani hapa kiongozi aliyekukosea

Mimi nasema waliouza Masaki na Oysterbay kwa kujuana na kwa hela mbuzi sana , hii imewakatili vizazi vingi kutoishi maisha niliyowahi kuishi

Sijui huko mikoani kama bado kuna maeneo yaliyoitwa uzunguni yenye nyumba za vigae vya mkoloni kama bado kuna nyumba za serikali
 
Mimi naanza.

•Alaaniwe kiongozi aliyeuza nyumba za serikali kwasababu yoyote ile. Nyumba zile ni za watumishi wa kawaida, wakaziuza kisha watumishi wakaanza kuishi kifukara lakini wao wenyewe waliishi nyumba za bure. Watumishi kutokana na vipato vyao hawawezi kupata viwanja vya milioni 30 hivyo wananunua viwanja vya milioni 2 maporini kisha pesa nyingine wanaanzia ujenzi.

Baadaye shida inakuja muda na gharama za kufika kazini . Sababu zao mfu eti ni gharama kuziendesha. Kwani kila nyumba ikifungwa mita ya maji na umeme kisha kila mtumishi ajilipie mwenyewe kuna tatizo?

Service ya rangi ifanywe na mtumishi mwenyewe na ikiwa atahamishwa kwenye nyumba husika ndani ya miaka 3 baada ya kupaka rangi serikali itaangalia namna ya kum refund kidogo na ikiwa ataishi zaidi ya miaka 3 basi hakuna refund.

• Alaaniwe aliyeizika Tanganyika huku Zanzibar ikiendelea kung'ara. Wote waliohusika vizazi vyao vilaaniwe.

•Alaaniwe kiongozi yeyote aliyehusika kuleta kikokotoo cha hovyo na kuzuia fao la kujitoa. Yeye mwenyewe kajitoa nje ya alichokileta kwa watumishi licha ya kukisifia kuwa ni chema
Nikiwataja hapa itakuwa nouma lakini.. Mungu yupo na walipanda vyeo sababu yakukomesha mimi..
 
Walaaniwe Viongozi wote wanaojilimbikizia mali kwa kuvuja mali za umma na wanaowatoa wengine kafara ili wapate vyeo au wabaki madarakani.
 
Back
Top Bottom