KERO Mlangarini Sekondari (Arusha) mnazuia Vyeti vya Wanafunzi kwa Sheria au Kanuni ipi?

KERO Mlangarini Sekondari (Arusha) mnazuia Vyeti vya Wanafunzi kwa Sheria au Kanuni ipi?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mzazi niliye Arusha, mtoto wangu amehitimu kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Mlangarini, iliyopo Arumeru. Nimejikuta kwenye hali ya sintofahamu na masikitiko makubwa kuhusu jambo lililotokea baada ya watoto kumaliza masomo yao.

Kinachonisikitisha ni kwamba, kuna wanafunzi 21 tu waliotajwa kuhusika na uharibifu wa mali. Lakini cha kushangaza, shule inadai kila mwanafunzi aliyehitimu—jumla yao wakiwa 265—alazimike kulipa shilingi 125,000 ili aweze kupewa cheti chake.

Najiuliza, huu uamuzi umetoka wapi? Na kwa nini adhabu ya watu wachache ibebwe na wanafunzi wote?


Zaidi ya hapo, malipo hayo yanadaiwa kufanywa kwa njia ya simu, jambo linalozua maswali zaidi kuhusu uwazi wa mchakato mzima. Hakuna maelezo rasmi wala ushirikishwaji wowote kwa wazazi. Tumeshtuka tu watoto wanapokwenda kuchukua vyeti wanaambiwa wazi kabisa—bila kulipa, hupati cheti.

Kwa maelezo tuliyoyapata, uharibifu uliotokea ulikuwa ni wa wanafunzi wenyewe kwa wenyewe—kidato cha nne kuharibu mali za kidato cha tatu, na kidato cha tatu kufanya vivyo hivyo. Hii si mali ya shule, bali ni ya wanafunzi.

Sasa tunashindwa kuelewa:
  • Kwa nini wanafunzi wote wanawajibishwa kulipa?
  • Kwa nini wazazi hatukushirikishwa katika maamuzi haya?
  • Kwa nini cheti kinazuiwa kwa sababu isiyoeleweka wazi?
  • Je, huu ni utaratibu halali kwa shule ya serikali?
Hali hii inaumiza sana kama mzazi. Tunaona kama kuna dhuluma na ukosefu wa haki kwa watoto wetu.

Naomba mamlaka husika ziingilie kati kwa haraka:
  • Kuchunguza uhalali wa malipo haya.
  • Kuzuia vitendo vya kuzuia vyeti kwa wanafunzi bila sababu za kisheria.
  • Kuhakikisha haki na uwazi vinazingatiwa katika shule za serikali.
Tunaomba sana sauti yetu isikike.
 
Back
Top Bottom