A
Anonymous
Guest
Geti la kutokea Daladala kwenye Stendi Kuu ya Nyegezi kwenda Barabara Kuu (highway) ndilo hilohilo linatumika kama njia ya abiria kupita wakiwa wanaingia kutoka upande wa barabara kuu, kibaya zaidi ni kuwa upo mlango wa abiria kwa upande huo lakini umefungwa na kuwalazimu abiria wote wanaoingia kutokea barabara kuu au wanaotoka wapite njia moja na daladala zinazotoka stendi kwenda barabara kuu.
Hali hii imekuwa ikileta usumbufu, mianya ya wizi wa mizigo ya baadhi ya abiria wanaosafiri maana vibaka wanaojificha kwenye kimvuli cha udalali wa tiketi wamekuwa wengi ukishuka tu wanakupokea kama sio mzoefu utaibiwa tu.
Naomba mamlaka husika ama ifungue mlango wa abiria kupitia au izuie kabisa abiria waipite kwenye mlango wa kupitia Daladala, la sivyo tutakuja kutafuta suluhisho baada ya ajaLi kutokea maana Daladala wanapita kwa fujo mahali hapo wakiamini abiria ndio wameingia kwenye njia yao.