Mlenda wa unga unatokana na majani gani na yanapatikana wapi?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Kuna ule mlenda huwa unapikwa kutokana na majani fulani yanayosagwa kama unga, unaitwa mlenda wa unga.
Haya majani yanayotengeneza huu mlenda wa unga yanapatikana wapi?
Yanauzwa sokoni kama mboga ?
Unaweza kuyapikia mlenda yakiwa mabichi(hayajakauka) kama mboga nyingine za majani?
 
 

Attachments

  • FB_IMG_1704570531581.jpg
    124.7 KB · Views: 2
Yes,
tena sasa hivi yamechopua vizuri yana ukijani wa kuvutia mno na mlenda wake ni mtamu ya ule wa unga.

Infact,
ukichumwa ukiwa mbichi, hasa nyakati za mavuno, hukaushwa vizuri juani na kisha huhifadhiwa vyema kwenye mfuko hii hii ya salfeti, ndipo kwa wakati muafaka ikihitajika husagwa na kua huo wa unga wa mlenda.

Nadhani kwenye mashamba yangu umeota vizuri sana, lakini pia sijaona shamba la mtu ambalo halijaota mlenda hapa kijijini kwetu,
infact sasa hivi mlenda umeota hadi nyumbani 🐒
 
Huo mlenda unaitwa irimbe au maimbe, unatokana na majani ya mlenda yaliyochanganywa na majani ya maboga yakatuangwa au kusagwa kupata unga. Ni mboga tamu sana ya kienyeji. Ongeza ladha kwa kuweka maziwa au samli utakula ugali mpaka tumbo liwe kubwa haukinahi
 
Umesahau karanga zilizokaangwa na kusagwa vema/ntwili.
 
Yakikauka yanatengeneza mlenda bila bamia ila yakiwa mabichi ili yatengeneze mlenda inabidi kutumia na bamia?
Hayo majani ya maboga au msusa yakiwa mabichi unapika mlenda kwa kuchanganya bamia au majani ya mlenda yanaitwa malendi kwa kinyamwezi na ngogwe ukipenda, unaweza kuweka karanga laini ukipenda. Pili unaweza pika mzabagulo bila bamia.
Mswalu/nswalu au wapare wanaita msele ni majani ya maboga na malendi-majani ya mlenda aliyokaushwa na kusagwa hupikwa na kuwekwa karanga laini- ntwili. Ni rahisi kuandaa mwenyewe.
 
Kumbe hata huo wa unga huwa wanachanganya na majani ya maboga!
 
Mlenda wa kuchanganya majani ya maboga na bamia naujua vizuri, huu wa unga ndio siufahamu vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…