Wana singida na dodoma...
Wanaita irende au nswalu kwa wanyamwezi,
Majani yake ni kama majani ya mmea wa ufuta...
Yaaani kama unavyouona mmea wa ufuta na huo mlenda uko hivyo hivyo unafanana 90%
Cha kufanya kama ukiuona chuma majani yake uloweke kwenye maji...utaona yana toa mlenda mwingi na mzito ukiushika tofauti na majani ya mmea wa ufuta.
Hayo majani membamba ndo huanikwa yakikauka yana sagwa au kutwangwa na kutoa poda line tyr kwa matumizi ya mboga.
Ni tamaduni za ukanda wa kati wao wanategemea mvua ya msimu wa masika tu kwa hivuo mboga mbichi hupatikana kwa wingi kipindi cha mvua kwa hivyo ili kuhifadhi mboga kwa msimu wa kiangazi.
Walikuwa wana kausha mboga mbali mbali ikiwemo
huo mlenda,majani ya kunde(nyafwe/safwe)Chipali,Chiwandagulu,mitanda( nyama)nk
bila kusahau nyanya mshenzi na matango n.k pia nayo yalikuwa yanakaushwa juani na kuhifadhiwa.
Ukanda Juu kusini na mikoa ya Pwani hawajui mambo hayo kwa sabb wao wanapata misimu miwili ya mvua..
Kwaivyo mbogamboga na viungo fresh hawaishiwi kabisa.
Kumbuka si hivyo tu mpk viazi vitamu humenywa na kuanikwa kwaajili ya kuhifadhi kwa matumizi ya kiangazi.
Huitwa Michembe,yakichemshwa na kuanikwa yanaitwa matoolwa(matoborwa)
Ni matunda pekee sijawahi ona yaliyohifadhiwa kwa kuanikwa kama yapo watasema wakongwe.