Mlenda wa unga unatokana na majani gani na yanapatikana wapi?

Mlenda wa unga unatokana na majani gani na yanapatikana wapi?

Kwakweli ugali unashuka balaaa. Halafu ukute mrenda umelala( ulipikwa Jana yake usiku) then asubuhi upike ugali unakula unaenda kuchunga. 😀😀😀😀
😀😀 wa kulala balaa haupashwagi huo.
Upate na mhopopoto grass moja imemixiwa na mtumba ,au umekosa maziwa basi uchanganye mchuzi wa nyama kwenye mlenda.
Hatari na nusu...hata ule wiki zima haukinai.
 
nikiona mlenda au bamia ule mvutiko wake huwa najenga picha mbaya sana akilini japo unamanufaa mengi mwilini ila siukubali kabisaa
 
Kuna ule mlenda huwa unapikwa kutokana na majani fulani yanayosagwa kama unga, unaitwa mlenda wa unga.
Haya majani yanayotengeneza huu mlenda wa unga yanapatikana wapi?
Yanauzwa sokoni kama mboga ?
Unaweza kuyapikia mlenda yakiwa mabichi(hayajakauka) kama mboga nyingine za majani?
Porini
 
Katika mboga ambayo ilipikwa kwa kila namna lakini nilishindwa kumaliza hata tonge mbili ni hayo mamilenda mboga ilinishinda tangu utoto mpaka sas hv sion ladha yake kabisa kabisa.
 
Kuna ule mlenda huwa unapikwa kutokana na majani fulani yanayosagwa kama unga, unaitwa mlenda wa unga.
Haya majani yanayotengeneza huu mlenda wa unga yanapatikana wapi?
Yanauzwa sokoni kama mboga ?
Unaweza kuyapikia mlenda yakiwa mabichi(hayajakauka) kama mboga nyingine za majani?
Majani pori
Hayapo kila sehemu,, Yapo maporini huko nikipita nitaileta picha yake.
 
Kuna ule mlenda huwa unapikwa kutokana na majani fulani yanayosagwa kama unga, unaitwa mlenda wa unga.
Haya majani yanayotengeneza huu mlenda wa unga yanapatikana wapi?
Yanauzwa sokoni kama mboga ?
Unaweza kuyapikia mlenda yakiwa mabichi(hayajakauka) kama mboga nyingine za majani?
Unatokana na majani ya matango asili au mihogo.

Majani huwa yanachumwa mabichi yanakaushwa kwa jua kisha yanahifadhiwa kwa matumizi.

Pishi lake lazima lichanganywe na karanga kuleta ladha na uzito.

Kwa majani ya matango yanaweza kutengeneza mlenda yakiwa mabichi kwa kuchanganya na bamia au mlenda pori wasukuma wanaita twege, makonda au bhunani.
 
Majani ya maboga, majani ya matango ya kienyeji (Limbe kwa Kisukuma) yanachanganywa na mmea mmoja huwa unateleza fulani hivi jamii ya Malvaceae. Kwa hiyo unaweza kuamua kukausha ya maboga peke yake unachanganya na hayo majani teleza, au matango ya kienyeji peke yake unachanganya na hayo majani teleza..Hii ikipikwa na kuwekwa karanga inakuwa balaa! Kwa Kisukuma tunaita Nzubo!
 
Singida ndalu hiyo, otherwise ni bamia tu.
Kula bamia why complicate things.
Mtu una uwezo kuhangaishana na vyakula vya kijijini ambavyo wanakula watu duni huko porini vya nini?
Kwanza hata hujiskii utakua unawazulumu?
Kunywa supu ya bamia fresh, unapika na chumvi mixer kidogo tu unapata mlenda.
 
Back
Top Bottom