Mlenda wa unga unatokana na majani gani na yanapatikana wapi?

Mlenda wa unga unatokana na majani gani na yanapatikana wapi?

Nyanya mshenzi ndo zile ndogo? Ila umeongea ukweli mtupu. Mihogo-makopa, pilipili, uyoga, nyanya na ngogwe zote hukaushwa.
Yes ni vinyanya vidogoo sana.
Vilijulikana hivyo sehemu nyingi.
Kwa vyakula hivyo na namna ya uhifadhi watoto wa 2000 hawaelewi chochote.
Tumetoka mbali sana.
 
Huo wa Inga hutokana na mlenda WA asili AMBAO huitwa MBATA Unaoatikana Kwa wingi DODOMA kati.ni mzuri na mtamu pia unavirutubisho vingi kuliko wa bamian na maboga
 
Kuna ule mlenda huwa unapikwa kutokana na majani fulani yanayosagwa kama unga, unaitwa mlenda wa unga.
Haya majani yanayotengeneza huu mlenda wa unga yanapatikana wapi?
Yanauzwa sokoni kama mboga ?
Unaweza kuyapikia mlenda yakiwa mabichi(hayajakauka) kama mboga nyingine za majani?
Naam, yakiwa mabichi yanapikwa mlenda pia.

Huo mlenda wa kusagwa unaitwa 'nswalu'.

Unatokana na majani ya mmea unaoitwa mlenda, mmea huo unafanana na mmea wa ufuta pamoja na majani ya matango pori.

Ama kwa kutumia bamia pamoja na majani ya maboga.

Majani hayo huchumwa na kukaushwa kwa kuchanganywa pamoja ama kwa kutenganishwa na kuhifadhiwa.

Maandalizi yake ni kusaga pamoja huo mchanganyiko, tui la karanga kwa pembeni.
 
Inaonekana wengi hawaufahamu vizuri mlenda aliouulizia mleta mada, yale ni majani mwitu ya aina moja hayajachanganywa na majani mengine, na pia inawezekana kupikwa yakiwa mabichi, au yakiwa yamekaushwa na kusagwa kua unga, na yanapatikana zaidi mkoa wa dodoma.
 
Mkuu safi sana kwa kuweka hii, ndugu mleta mada aya majani ya huu mlenda wa unga yapo jike na dume kuna huu ambao mdau kauposti ni jike kuna majani mengine ambayo ni dume, aya unakausha kwa kutumia jua alafu unachanganya na majani ya maboga ambayo nayo ukaushwa pia aya maboga huitwa malumbu.
Baada ya hapo twanga vyote kwa pamoja alafu chekecha utaona mambo yalivyo na ugali wako wa Dona๐Ÿ˜‹๐Ÿ˜‹๐Ÿ˜‹๐Ÿ˜‹
Kingine aya majani ya mlenda msimu wa mvua ndio huwa yanachipua kwa wingi sana.
 
Asee hii nchi kweli ni kubwa...
Maana ya mlenda ni KITU chochote kinachoteleza... (Utajua mwenyewe)
Nilivyomwelewa mtoa mada faster nilijua anazungumzia mboga maarufu kwa sisi wenyeji wa Iringa na Njombe, maarufu kama MKUNUNGU...
Hii mboga haichanganywi chochote wakati wa kuandaa, na ni mboga pori, inaota kama vichaka kwenye udongo wa mfinyanzi, mashina yake Hadi majani Yana miba, haikui kuwa miti mikubwa sana hapana. Ni kama ilivyo mimea ya ndula.
Majani yake yakiwa mabichi Yana aroma kama ya Limau hivi, na haiandaliwi Toka kwenye majani mabichi, isipokuwa yaliyokaushwa kwenye kivuli na kusagwa. UNGA wake hubaki na ule ukijani wake wa ASILI.
MBOGA HII HAICHAGUI MAPISHI WALA KIUNGO... NA INA MATCH NA KILA CHAKULA, AROMA YAKE YA CITRUS IKIWA NI APPETIZER MUJARABU KABISA.
-kamwene mbemuli-
Mlenda wa huku ni tofauti, unaota porini pia ila unakua kama majani ya kawaida madogo madogo siyo mti. Unafanana na hiyo picha aliyoweka mdau.

Hatua za kupika sizijui, mwenye salio apige nimuulize mama unapikwaje, Akipika mama ni๐Ÿ˜‹, ila akipika bibi ni very๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ sahani haioshwi, inalambwa...
 
Nswalu hiyo kisoda kimoja tu ,kinajaza sufuria nzima ,we ni kuongeza maji.Siupendi.
 
Mkuu safi sana kwa kuweka hii, ndugu mleta mada aya majani ya huu mlenda wa unga yapo jike na dume kuna huu ambao mdau kauposti ni jike kuna majani mengine ambayo ni dume, aya unakausha kwa kutumia jua alafu unachanganya na majani ya maboga ambayo nayo ukaushwa pia aya maboga huitwa malumbu.
Baada ya hapo twanga vyote kwa pamoja alafu chekecha utaona mambo yalivyo na ugali wako wa Dona๐Ÿ˜‹๐Ÿ˜‹๐Ÿ˜‹๐Ÿ˜‹
Kingine aya majani ya mlenda msimu wa mvua ndio huwa yanachipua kwa wingi sana.
 
Attachments

  • FB_IMG_1704570536983.jpg
    FB_IMG_1704570536983.jpg
    143.8 KB · Views: 2
  • FB_IMG_1704570527134.jpg
    FB_IMG_1704570527134.jpg
    111.3 KB · Views: 3
Yes,
tena sasa hivi yamechopua vizuri yana ukijani wa kuvutia mno na mlenda wake ni mtamu ya ule wa unga.

Infact,
ukichumwa ukiwa mbichi, hasa nyakati za mavuno, hukaushwa vizuri juani na kisha huhifadhiwa vyema kwenye mfuko hii hii ya salfeti, ndipo kwa wakati muafaka ikihitajika husagwa na kua huo wa unga wa mlenda.

Nadhani kwenye mashamba yangu umeota vizuri sana, lakini pia sijaona shamba la mtu ambalo halijaota mlenda hapa kijijini kwetu,
infact sasa hivi mlenda umeota hadi nyumbani ๐Ÿ’
Gentleman, nasikia ukila mlenda kisawasawa unakuwa na makalio laini na matamu kama Poshi Queen.

Hii imekaaje?
 
Yes,
tena sasa hivi yamechopua vizuri yana ukijani wa kuvutia mno na mlenda wake ni mtamu ya ule wa unga.

Infact,
ukichumwa ukiwa mbichi, hasa nyakati za mavuno, hukaushwa vizuri juani na kisha huhifadhiwa vyema kwenye mfuko hii hii ya salfeti, ndipo kwa wakati muafaka ikihitajika husagwa na kua huo wa unga wa mlenda.

Nadhani kwenye mashamba yangu umeota vizuri sana, lakini pia sijaona shamba la mtu ambalo halijaota mlenda hapa kijijini kwetu,
infact sasa hivi mlenda umeota hadi nyumbani ๐Ÿ’
Kumbe umeathiriwa na mlenda ndio maana una...
 
Inaonekana wengi hawaufahamu vizuri mlenda aliouulizia mleta mada, yale ni majani mwitu ya aina moja hayajachanganywa na majani mengine, na pia inawezekana kupikwa yakiwa mabichi, au yakiwa yamekaushwa na kusagwa kua unga, na yanapatikana zaidi mkoa wa dodoma.
Basi kila sehemu na taratibu zake.

Mlenda wa Singida, Tabora na Shinyanga, hutengenezwa kwa kutumia majani ya mmea wa mlenda pamoja na majani ya matango pori ama msusa(majani ya maboga).
Mchanganyiko huo ndiyo huzaa 'nswalu' yenye hadhi.

Usipochanganya jani la mlenda ama bamia mboga hiyo haitaweza kulendemka na kuwa kitu kingine.

Kina mama mko wapi msaidie ufafanuzi wa hii issue!

Nimekazana kutetea utadhani naingiaga hata jikoni kwenyewe!
 
Back
Top Bottom