Mlengo na ukomavu wa Mama Samia utaonekana kwenye uteuzi wa Makamu wa Rais

Mlengo na ukomavu wa Mama Samia utaonekana kwenye uteuzi wa Makamu wa Rais

Automata

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2015
Posts
3,414
Reaction score
4,794
Kwenye uteuzi wa makamu wa raisi ndipo patajulikana mlengo na ukomavu wa Mama Samia

Kama ni mtu sahihi wa kuendeleza kazi za mtangulizi wake ama la!; ikiwemo miradi mikubwa

Kama yupo kwa ajili ya hapa kazi tu ama la!

Kama yupo kwa ajili ya vita ya rushwa, ubadhilifu, uzembe, uvivu ama la!

Kama yeye ni CCM na Tanzania mpya kweli aliyokuwa akiijenga na kuihubiri mzee ama CCM ya zamani/asilia/watoto wa mjini

Na kadhalika na kadhalika
 
Mama Samia atachaguliwa VP na kundi flani ndani ya CCM. JK keshatia mkono wake hapo now that Mkapa (na JPM) hawapo

The best Rais can do ni kuomba tu apewe choices mbili ili labda achague the “lesser devil”. Otherwise hana influence hata ya 40% nani awe VP
 
Pls NEVER EVER underestimate --- msimhafilishe --- Rais Samia. She is President na nusu. If JPM was Chuma cha Dhahabu, hers is Chumu ya Almasi; JPM was Chuma, hers is Iron Lady. 🙂

NB: Tuomboleze kwa amani, utulivu, mshikamano na kujihadhari!
 
Hakuna sababu ya ulazima Mh Rais afuate mambo ya mtamgulizi wake, Infact mengi yalikua si ya kuigwa ukiondoa miradi mikubwa na ujenzi wa miundombinu.
 
Mangula na Shein, makamu wenyeviti wa CCM, ndio watakaoamua ni nani awe VP, presida madam ni rubber stamp tu.

Kama Mangulla na Shein watahakikisha Kikwete hawaburuzi cc kwa maslahi yake na sio ya nchi; ikumbukwe kuwa Rais Samia anahitaji mtu wa kuhakikisha kuwa ILANI ya ccm inatekelezwa.

Wako wanaccm ambao walisjhiriki na marehemu na rais Samia kuiuza Ilani ya ccm kwa wananchi hivyo wapewe nafasi ya kumsaidia Rais kuitekeleza.
 
Huu ni ukweli mchungu. JPM litengeneza mfumo mbovu was utawala na uongozi ,itachukua miaka mingi kulirekebisha.

Ukijumlisha na ubovu was Katiba.

Makundi ndani ya CCM.

Majeruhi wa ubabe wa JpM.

Mama anahitaji maombi!

Otherwise atakubali yaishe!

Mkapa na kundi lake walikuwa wanaiendesha nchi Kama vile watakuwepo milele!

Sasa mliowadharau ..JKs ndio wametamaliki!

Mungu tuvushe!
 
Mama Samia atachaguliwa VP na kundi flani ndani ya CCM. JK keshatia mkono wake hapo now that Mkapa (na JPM) hawapo

The best Rais can do ni kuomba tu apewe choices mbili ili labda achague the “lesser devil”. Otherwise hana influence hata ya 40% nani awe VP
Itakuwa shida sana
 
Kama Mangulla na Shein watahakikisha Kikwete hawaburuzi cc kwa maslahi yake na sio ya nchi; ikumbukwe kuwa Rais Samia anahitaji mtu wa kuhakikisha kuwa ILANI ya ccm inatekelezwa. Wako wanaccm ambao walisjhiriki na marehemu na rais Samia kuiuza Ilani ya ccm kwa wananchi hivyo wapewe nafasi ya kumsaidia Rais kuitekeleza.
Mkuu kutekeleza au kuijua Ilani na Uongozi ndani ya CCM ni Mbingu na Ardhi!
 
Sina Imani kabisa na mama samia.. Najua anajaribu bahati yake,

Tatizo magufuli ameacha baraza changa sana, baraza tegemezi, lisilo na maamuzi, maamuzi yote alikua anafanya Magufuli.
Uwezo wanao sema jamaa aliwatisha sana pamoja na kuchukua bongo zao, aliweka mfumo wa kila kitu aulizwe yeye tu.
 
Pls NEVER EVER underestimate --- msimhafilishe --- Rais Samia. She is President na nusu. If JPM was Chuma cha Dhahabu, hers is Chumu ya Almasi; JPM was Chuma, hers is Iron Lady. 🙂

NB: Tuomboleze kwa amani, utulivu, mshikamano na kujihadhari!
We are not underestimating our Madame Rais!
But the atmosphere she is facing ahead ....😓😓😓😓😓
 
Hiyo ndio sababu wengi wanaitaji katiba ambayo itaunda mifumo thabiti ifike hatua hata mwehu akipewa nchi bado katiba inampa muongozo na ikitokea ameboronga anawajibishwa.
Narudia kusema haya mambo ya kuona katiba ni suluhisho, tutachelewa sana. labda huko ulaya na marekani si africa. Sisi bado tunahitaji strong leaders not strong katibas. Mjue hakuna inchi africa hii yenye katiba bora na ya kisasa kama kenya. Lakini bado walimtaka magu hata kwa mwaka mmoja tu.
 
Hizo ni propaganda za Mataga
 
Sifa moja ya kiongozi ni kuwa na msimamo.Rais Samia napaswa kuteua mtu anayemwamini lakini ikiwezekana asiwe mtu mwenye jina kubwa ili aweze kuchapa kazi vizuri.Akiteua wale wenye majina wengi Wana ndoto ya 2025 watamvuruga Sana .Pia asiwaachie wazee wastaafu wamuamulie, Bali awaombe tu ushauri.
 
Kesha sema yeye ndio Rais, ingawaje tumeona ameapishwa, na kwa kitendo hicho yeye ndiye Rais!

Back
Top Bottom