Mlete mzungu: Uzi wa picha za mzungu wa Simba kwenye pozi tofauti

Utani wa hivi katika soka unafanyika dunia nzima labda uanze kushabikia soka jana,au kisa huyo ni mzungu ndani ya ardhi yako ya Tz? acha inferiority complex
Mkumbushe haland alivyo pondwa pale England.....baada ya mechi yake ya kwanza
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ushabiki unabmambo na msikasirike huo ni utani wa jadi kwahyo hapo habaguliwi mtu watani lazma wataniane
Maisha simple Sana mkuu[emoji23][emoji23]
 
Hii sio sawa kabisa!
Mimi sio mshabiki wa simba hata kidogo ila huu uzi ni wa KIBAGUZI!
Kila siku tunalaani ubaguzi kwenye soka Ulaya sasa tusilete huku nyumbani kivingine
ungesema wachezaji wa simba angalau ila sio kumlenga mtu moja kwa moja kama una bifu naye!!!
 
Mzungu anatrend kama Mandonga mtu kazi
Hii bongo ......ukifaulu watu wanaanza majungu

But
Anguko lako ndio furaha yetu
Kama mandonga mtu kaziiii[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Mtoa mada ni Yanga mwenzangu! Ila katika hili la huyu mshambuliaji wa wapinzani wetu, aisee sikuungi mkono.

Angefanyiwa hivi Samatta kule Ubelgiji, Uingereza, au Uturuki! Tungelaani sana. Hivyo kuna baadhi ya mambo tunatakiwa kuwa fair.

Ingawa na wanamsimbazi pia mwakani mtafute Mshereheshaji wa kueleweka. Achaneni na MC wa kubabaisha kama Ahmed Ali! Huu ujinga wote ulianzia kwake. Alikuwa na sababu gani ya kumtambulisha kama Mzungu, badala ya jina lake? Hii nchi imeshavurugwa kitambo! Ona sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…