Mlichotufanyia Bus la Mghamba, Arusha-Kahama ni kitendo cha kinyama. Serikali itazameni kampuni hii

Mlichotufanyia Bus la Mghamba, Arusha-Kahama ni kitendo cha kinyama. Serikali itazameni kampuni hii

Tumefika Singida mbele kuelekea Misigiri gari ikaharibika. Kondakta alitokomea kwenda mjini na abiria tukawa tumetelekezwa. Jirekebisheni
Kwahiyo mpaka muda uliokuwa ukiandika huu Uzi wako ulikuwa bado Umetelekezwa Porini hapo Misigiri / ulijiongeza na ukaomba Hifadhi huko?
 
Nlichukua usafiri mwingine baada ya kutelekezwa masaa 6,uzi huu nimeandika nkiwa geto Kahama kwa uchungu kabisa.
 
Asante,na pia tunawaanika huku ili wajirekebishe,mtu ulipe nauli mara mbili,usawa wenyewe huu wa January
 
Tumekua THIMBA tun'goe siti?
 
Waliobaki walikua na majibu ya ukali na matumaini ya uongo
Hamjui sheria? Hamkuwa na namba za Sumatra/LATRA, au Police? Pia jitahidini muwe mnasoma na sheria za usafirishaji zinasemaje kuliko kuwa bise kusoma makala za udaku pekee.

Mngekuwa mnajua sheria zinasemaje msingepata shida, na wao hao wenye kampuni ni wajanja sana wanawafanyia hivyo kwa sababu wanajua hamjui sheria za usafirishaji abiria zinasemaje
 
Kuna basi linaitwa Ngwelu Tabora -Bunda likifika Mwanza saa 10jioni linapakiza abiria wa Musoma mkifika Bunda mnafaulishwa kwenye basi la Continental (Mwz-Msm).
Juzi Kati tulikuwa zaidi ya abilia 90+, hii haikubaliki hata kidogo.
Mnao panda mnakuwa wajinga ndo maana, wanafanya hivyo kwa sababu abiria wako kama kondoo, mimi huo moto nitakao uwasha hapo watanikodoshia gari la private, mnakuwa wapole mno nidhamu za uoga,
 
Nlichukua usafiri mwingine baada ya kutelekezwa masaa 6,uzi huu nimeandika nkiwa geto Kahama kwa uchungu kabisa.
Aisee mna nidhamu za uoga mno sasa umekuja kulalamikia huku iweje? Uwe unatumia muda some time kusoma soma sheria, mnadhurumiwa kwa sababu hamjui sheria, mnabakia kulalamika tu
 
Abiria nazsni asilimia 99 hasajui haki zao, kama wapo wanao jua ni asilimia 1 tu na wenye mabasi wanatumia sana huo muanya wa abilia kuto kujua chochote,
 
Back
Top Bottom