Tofauti kati ya awamu ya kwanza ya mwl Nyerere na awamu hii ya tano kipindi cha pili ya SSH ni kwamba:
Mwalimu Nyerere aliwaondoa wananchi kutoka kwenye ardhi yao ya asili na kuunda vijiji vya ujamaa lengo likiwa kupata huduma za maji, zahanati na shule za kijiji. SSH ameondoa wamasai kutoka kwenye ardhi yao ya asili na kupelekwa maeneo ya Tanga yawezekana lengo likawa lile lile kama awamu ya kwanza.
Hata kabla hatujapata muda wa kutosha kutafakari haya masuala mazito yanayogusa maisha wa wananchi ambao ndio wamiliki wa ardhi ya Tanzania na sio Serikali, Linakuja suala la Bandari kukabidhiwa kwa wageni kwa kisingizio cha kufanya maboresho na kuongeza mapato..... Hii haikubaliki!
Kama hatuna uwezo wa kuendesha bandari zetu wenyewe kwa sasa, kwa nini tusisubiri hadi hapo watoto wetu walioko mashuleni wapate akili ya kusimamia rasilimali ambazo ndio urithi wa taifa hili? Haraka hii ni ya nini hasa wakati tuliisha chelewa?.... Nawaza tu!. Namaste.[emoji120]