DOKEZO Mlima wa Morogoro unaungua, Serikali ya Mkoa ingilieni kati

DOKEZO Mlima wa Morogoro unaungua, Serikali ya Mkoa ingilieni kati

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kuna chuo cha maafisa wa polisi Kidatu kipo kule, kuna bwawa la umeme la Kidatu kuna kabila la Wavidunda wapo kule, kuna wanyama, kuna safu za milima ya Udzungwa kule
 
Njoo mitaa ya huku highlands ndio utapata picha vizuri
Uko wapi mkuu ipige basi uitume mimi nimeipiga tokea kilakala ila huo ni mlima unaoinamia chuo cha ualimu kigurunyembe.
 
Kuna chuo cha maafisa wa polisi Kidatu kipo kule, kuna bwawa la umeme la Kidatu kuna kabila la Wavidunda wapo kule, kuna wanyama, kuna safu za milima ya Udzungwa kule
Hii location ni uelekeo wa mikumi mkuu huu moto uko hapa mjini manispaa.
 
Moro ilikua moro bwana miaka ya 90 nimekaa pale na kusoma. Milimani maji yanatililika asubuhi ukiongea unatoa mvuke dah....palikua patam hatari imefika 2000 mara mlima uwake moto mara ghafla maji kule juu huoni yanatililika mpaka mto morogoro unakauka watu wamevamia milimani kata miti haribu mazingira ...so sad...
 
Muda huu mlima wa morogoro unaungua naiomba serikali iingilie kati mkuu wa mkoa tuma timu ikazime kwakweli inaumiza sana kwasisi wapenda mazingira.
Kabisa zamani miaka ya 1998 nikipita hapo mjini kwenda Mzumbe mandhari ilikuwa nzuri sana lakini watu wamekuwa wakiishi milimani na kuchoma moto misitu udongo unaporomoka na miamba imebaki wazi kweli inasikitisha sana!
 
Back
Top Bottom