DOKEZO Mlima wa Morogoro unaungua, Serikali ya Mkoa ingilieni kati

DOKEZO Mlima wa Morogoro unaungua, Serikali ya Mkoa ingilieni kati

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Moro ilikua moro bwana miaka ya 90 nimekaa pale na kusoma. Milimani maji yanatililika asubuhi ukiongea unatoa mvuke dah....palikua patam hatari imefika 2000 mara mlima uwake moto mara ghafla maji kule juu huoni yanatililika mpaka mto morogoro unakauka watu wamevamia milimani kata miti haribu mazingira ...so sad...
Ulikuwa Moro Kwa sehemu Gani mkuu maana na Mimi miaka hiyo nilikuwa Moro pia
 
Serikali ya Mkoloni German,uk walizuia shughuli zote za kibinadamu juu ya mlima, baada ya Uhuru ikawa ni uhuru bila kufuata sheria za mazingira na viumbe.

Ukiwa Msavu unaona kipande cha udongo ulio megeka. Lakini hakuna hatua zozote zilizo chukuliwa.
Tegemeeni maafa +.
 
Nimeuona huo moto kwa siku 3 mfululizo ,na kila siku unaongezeka.
Wachukue hatua,ikiendelea kwa siku nyingine zaidi panaweza kuungua kote(pamoja na watu) maana unaonekana sio moto mdogo.
Nasikia wanachoma wakiwinda vimnyama gani sijui huko juu.
Waluguru bana!
 
Back
Top Bottom