Utaona kwamba mifumo ya ulinzi kwa nchi nyingi za Afrika iko kutetea maslahi ya viongozi na utawala uliopo. Hawana lengo kuu la kulinda maslahi ya nchi, ndio maana wanahatarisha siri za nchi kuvuja kwa kusukumiza wenye nazo nje. Wapi utakuta DG mstaafu wa CIA, FBI, MOSSAD, FSB, M16 au shirika lolote la nchi kubwa duniani anaenda nje kuwa balozi.
Majasusi wote wana security clearance, ili awe mole au double agent lazima kwanza awe anaaminika kwao vinginevyo hatopewa kazi au atalishwa taarifa za uongo. Hiyo security clearance mbona isitumike kuishi nao hapa.
Tatizo kukaa nao nchini ni shida maana hutowapa house arrest bila sababu hivo watakuwa mtaani. Ila kuwapeleka nje ni shida kwa nchi.