Mlio jirani na Rais mshaurini; ni sawa kutoa zawadi lakini kutapanya pesa nyingi kiasi hiki hapana!

Jambo nzuri sana mm kama aongeze pesa kwenye budget ya michezo angalau huko kunaoneka impact yake kwa urahisi..
Viwanja vya michezo viboreshwe wavutie wawekezaji wengi kwenye michezo..
Itasaidia kutangaza nchi sana..
 
Ofisi ya Rais Hadi DC Huwa Ina pesa za mambo hayo ila Sasa kuwe na regulations isiwe kadiri tuu Kiongozi anavyojiskia
 
Kuna Clip moja nilimsikia late Magufuri akisema" Laiti Samia asingekuwa mwanamke basi Makamo wake angekuwa Husein Mwinyi" sasa hivi tusingekuwa na haya mashaka.
Hata huyo Magufuli nae alikuwa anatapanya sana pesa Kwa kugawa hovyo Kwenye ziara zake kutafuta umaarufu.
 
Kuna fedha za mfuko wa rais, hizo hata CAG haruhusiwi kuzikagua. Hizo ndio fedha zinazotumika kufanya chochote atakacho rais ili kujibrand, ikiwemo vikundi vya kumpamba, na hata ikibidi kuwa na kundi la watu wasiojulikana. Lengo la fedha hizi ni kumtakatisha rais hata awe anachemsha vipi.

Mara nyingi sheria ya fedha za aina hii hupendekezwa na kupitishwa na washauri wa serikali zilizopoteza ushawishi kwa umma.
 
Jambo nzuri sana mm kama aongeze pesa kwenye budget ya michezo angalau huko kunaoneka impact yake kwa urahisi..
Viwanja vya michezo viboreshwe wavutie wawekezaji wengi kwenye michezo..
Itasaidia kutangaza nchi sana..
Sasa Bajeti ya michezo iongezwe kwenye Wizara sio kutoa toa hela bila utaratibu
 
Hela zote ziwe na utaratibu wa matumizi hata kama CAG haruhusiwi kukagua.

CAG mwenyewe anazifikia taasisi chini ya 40%
 
Ofisi ya Rais Hadi DC Huwa Ina pesa za mambo hayo ila Sasa kuwe na regulations isiwe kadiri tuu Kiongozi anavyojiskia
Haya ndio madhara ya kupoteza ushawishi kwa umma. Unafanya chochote ili kujustfy kuwa bado unakubalika na umma. Hii naifananisha na yule mwanaume anayehonga sana na kuishia kuchunwa ili kulazimisha penzi.
 
Haya ndio madhara ya kupoteza ushawishi kwa umma. Unafanya chochote ili kujustfy kuwa bado unakubalika na umma. Hii naifananisha na yule mwanaume anayehonga sana na kuishia kuchunwa ili kulazimisha penzi.
Hizo pesa zipo sio lazima kwamba zitumike ku justify kukubalika, viongozi mara nyingi wanaalikwa na taasisi mbalimbali hizo taasisi zinaomba michango , unadhani Kiongozi atatoa mfukoni mwake Kwa kipato binafsi ataweza?

Ndio maana unaona hata wabunge wamewekewa mfuko wa Jimbo kwa kazi hizo hizo ila walauo wao ziko regulated.
 
Kuna mtu ameomba historia ya kweli ya mtu mweusi hamjampatia mpaka sasa
 
Uchumi wetu umekuwa imara acha atapanye au kwakuwa haumo kwenye mgao??!!! Kila siku mnatuhubiria uchumi umeimaraka sasa kuna tatizo gani kutapanya hayo mamilioni?? Bado kuna mabilioni ya kufundisha wananchi katiba yapo njiani. CCM hoyeee!!
 
Kukuza mpira peleka pesa kwenye Taasisi husika / Grassroot ili wadau wajue wapi wazipeleke na wapi panahitaji; Hayo mengine kama ni zake binafsi hata akiamua azipeperushe watu waziokote ni sawa lakini kama ni hizi zetu (our hard earned cash) haitakiwi atumie hata senti tano bila consultation kutoka kwetu...;

Its not only about the Cash bali its a matter of Principle...
 

Ungejua zinazotoka bila taarifa, ungejikalia kimya.
 
Mh Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania amekuwa ndani ya utumishi wa umma kwa muda mrefu sana, amefanya kazi maeneo mbalimbali,amekuwa mbunge kwa miaka mingi, amekuwa waziri,Amekuwa makamu wa Rais na sasa Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania.Hivyo kipato chake cha halali tu kinachotokana na mishahara yake hawezi kushindwa kutoa kiasi hicho cha fedha. Kiasi hicho hakimshindi hata kidogo kutoa na kuchangia kwa ajili ya kuwapa hamasa wachezaji wetu.

Lakini pia hatoi tu katika michezo bali amekuwa akichangia katika maeneo mbalimbali na kwa watu mbalimbali,hivi majuzi majuzi tu tuliona akimjengea nyumba mtoto mmoja hivi na kumpatia Tabasamu na matumaini.Rais samia kiasili ni mtoaji kwa kile akipatacho.

Rais samia ni kiongozi na Rais wa wote,ndio maana ukienda katika kila eneo lazima uone alama zake,lazima ukute mafanikio yake ,lazima ukute Tabasamu na matumaini yanayotokana na mikono ya Rais samia.kila kitu kina nafasi yake na umuhimu wake. Leo hii nchi kama Uingereza au Spain inapata mapato makubwa sana kupitia michezo,imelitambulisha Taifa lake kupitia uwekezaji mkubwa katika michezo, na ina kusanya na kuboresha miundombinu yake kupitia mapato ya michezo.

Michezo itatupatia na kuitangaza nchi yetu,itatuletea wawekezaji wakubwa,itatuletea watalii,itazalisha ajira kwa vijana Embu fikiria mtu kama Sadio mane Namna alivyo saidia nchini kwake hasa kijijini kwake kwa kujenga vituo vya afya,angalia mtu kama christiano Ronaldo namna alivyotoa heshima nchi yake ,leo hii mpaka anasaidia waganga wa tetemeko kule Morocco,.amefika hapo alipo kwa kuwa Taifa lake lilimpa hamasa ya kukuza kipaji chake. Angalia watu kama akina David Beckam.

Tusimkatishe Tamaa mh Rais ,tumpe moyo na kumuunga mkono. Kwani akichangia katika michezo, kwamba vituo vya afya vimesimama kujengwa? Shule zimesimama kujengwa, barabara zimesimama kujengwa? Hivyo vyote si vinaendelea? Si vinafanyika? Unakumbuka nchi ya Rwanda iliyoa kias gani cha fedha kwa club kutoka Uingereza kwa ajili ya kutangaza nchi yao? Vipi ingekuwa kwetu? Si tungepigaa Makele? Tuacheni nongwa kwa mh Rais ndugu zangu. Katika hili sioni kosa la mh Rais wetu
 
Acha chokochoko, mama anaupiga mwingi!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…