Mlio kwenye system mtujuze, ni kwanini mikataba inayoingiwa kati ya Serikali na entity nyingi ya kimataifa hufanywa kuwa siri kwa wananchi?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
Eti jamani, hasa nyie mlio kwenye system hebu tupeni mwanga kidogo; ni kwanini mikataba inayoingia serikali huwa inafanywa kiwa siri kiasi mwananchi wa kawaida hapaswi kabisa kujua.

Mathalani hii mikataba ya mikopo, ni kwanini msiiweke hadharani ili tujue masharti yake yakoje, why?
 
Namna tuu ya kupiga mkataba wa inchi why iwe siri as if ni wa mtu binafsi.
Wabunge wapo wapewe iyo nafasi kuudadavua huo mkataba izi siri kuna siku tutaja ingia shimoni kama zama za EPA RICH MONDI SYMBIONI
 
Imejaa utapeli..na mingi kuna 10% ya viongozi kwa maslahi yao sio ya taifa...ndio mana inafanyea siri.

#MaendeleoHayanaChama
 
Ipo siku Nchi itauzwa in Jobs voice
 
For national interests/maslahi mapana ya Taifa..
Si kila kitu chafaa kuwa wazi.,

Na raia wakipewa wana input gani ss zaidi ya kelele km zinazoendelea twitter kuhusu speech ya Mama?.!
 
System unayoisema nayo pia imeshaharibika Mkuu.
 
For national interests/maslahi mapana ya Taifa..
Si kila kitu chafaa kuwa wazi.,

Na raia wakipewa wana input gani ss zaidi ya kelele km zinazoendelea twitter kuhusu speech ya Mama?.!
We akili yako imelala sana...
Ivi unahamini mwananchi ndio mwenye nchi.. so unapo mnyima taarifa nyeti za nchi inakuaje? Hapo
Serikali yoyote inayowanyima wananchi wake taarifa basi hiyo siyo serikali ya wananchi
Wajibi wa serikali kwa mwananchi ni kuweka taarifa zote wazi kwa ajili ya maslahi mapana ya Taifa..siyo unakopa unajificha then likibuma unaachiaTaifa msala la madeni
Yasiyo na kichwa wala miguu
Mfano jiwe alikopa kununua ndege na kufanya miradi isiyotekelezeka kimikakati...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
For national interests/maslahi mapana ya Taifa..
Si kila kitu chafaa kuwa wazi.,

Na raia wakipewa wana input gani ss zaidi ya kelele km zinazoendelea twitter kuhusu speech ya Mama?.!
Hapo hakuna maslahi ya taifa, maana mtu anaenda anajikopea tu mihela kwa masharti anayoyajua yeye tu, hii sio sawa, mikataba hasa hii ya mikopo yenye masharti na riba za ajabu ajabu inaweza ikasababisha siku tukaja kupigwa mnada, mikataba iwe wazi sote tuisome na tuielewe, WaTanzania sio ng’ombe!!
 
Hahhaha
At your best ignorant behaviour
 
Haya subirini watawekea kwenye gazeti la Majira msome
 
Lin uliwahi kuwekewa wazi????Na vp huyo jamaa yako marehemu aliwahi fanya hlo????
Hebu msitupigie kelele SUKUMA GANG
 
Nchi haijawahi kuweka wazi mambo wanayofanya na haita tokea

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…