Utanisamehe nimekuwa mvivu kufanya concise summary, nimetape maandiko ya watu , lkn ni ya kweli
b 30 October 2011 HIJA KWA BIKIRA MARIA NYAKIJOGA:Lurdi ya Bukoba yafanyika hii Leo 30-10-2011 HISTORIA FUPI YA NYAKIJOGA KWA U...
allenmkongo.blogspot.com
Pata kuijua historia ya Nyakijoga
30 October 2011
HISTORIA FUPI YA NYAKIJOGA KWA UTAFITI a kituo cha Hija cha Parokia ya Mugana.
Wakati huo Parokia ya Mugana ilikuwa ikijiandaa kuadhimisha Jubilei ya Miaka 50 tangu ilipoanzishwa. Jubilei ilikuwa iadhimishwe mwaka 1955. Kituo hiki cha Hija kilianzishwa kwa madhumuni ya kushiriki kiroho katika maadhimisho ya Jubilei ya miaka 100 tangu tamko rasmi la Kanisa la mwaka 1854, kuwa ni nguzo ya imani kwamba Bikira Maria aliumbwa bila dhambi ya asili. Vilevile, mwaka 1958 kuliadhimishwa Jubilei ya miaka 100 tangu Bikira Maria mwenyewe alipomtokea msichana Bernadeta Subiru huko Lurdi Ufaransa mwaka 1858 na kujitambulisha kuwa yeye ndiye “aliyeumbwa bila dhambi ya asili”
Kwa kujitambulisha hivyo Bikira Maria athibitisha ukweli ambao ulikuwa unakubaliwa na Kanisa katika mapokeo yake ya kawaida (Tradition), ambao ulitamkwa rasmi na Kanisa mwaka 1854.
Ili kuwawezesha waumini wote wa Jimbo la Rutabo la nyakati zile kushiriki kikamilifu, Mwashamu Laureani Rugambwa, alimwomba Baba Mtakatifu Pio XII awaruhusu wote watakao Hiji hapa wapate rehema za Jubileo hiyo kuu ya Lurdi. Baba Mtakatifu aliruhusu.
.......................................................
Ijue Nyakijoga, Mugana, Kiziba, Bukoba, sehemu ya kuhiji ibada za Bikira Maria. Mwanzilishi ni Kardinali Rugambwa. Alipendelea kuhiji kwa Bikira Maria kule Leuge Ulaya. Lakini baadae alimwomba Pope John kupata sehemu ya kuhiji Afrika. Pope alikubali na safari ya kutafuta ikaanza. Kardinali alibaini sehemu ya Mugana iliyokuwa inatiisha kwa miamba yake kama mizizi na maji kuchipukia humo pangoni. Palitengenezewa sanamu ya Bikira Maria na Kanisa. Watu walianza kuhiji toka pande za dunia hadi leo hii. Hudaiwa hata maji toka pale yana miujiza ya mama Maria. Kwenye miaka ya sitini nilihiji nikiwa mkatoriki, lakini kwa sasa mimi Mpentekoste, siwezi kwenda tena eg Zaburi 115, 146 na Kutoka 20 nk . Soma kitabu cha maisha ya Mhadhama Kardinali Rugambwa toka Bukoba