Mlioacha kutumia pilipili mliwezaje? Licha ya kunidhuru kila ninapotumia nimeshindwa kabisa kuacha ulaji wake

Pilipili ni dawa ya mafua na kikohozi
Hata mimi nahisi maana nikila kifua kinabata vaibu fulani kama kinapona lakini huwa temporary ..
 
Kweli mzee source ipi ?
Mkuu km unavuta sigara acha
Then pilipili ukipika mboga uingize ndani ya Mboga , usitoboe Mkuu acha Mboga ichemke vizuri so hapo probably utakuwa umeipunguza Nguvu . Usitumie pilipili mbichi .
 
Chakula bila pilipili naona kama chakula cha mtoto mchanga..siwezi kula kwa raha..kwangu mimi pilipili nikiungo kikubwa sana kwenye chakula kuliko hata chumvi.

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu km unavuta sigara acha
Then pilipili ukipika mboga uingize ndani ya Mboga , usitoboe Mkuu acha Mboga ichemke vizuri so hapo probably utakuwa umeipunguza Nguvu . Usitumie pilipili mbichi .
Sigara sivuti kabisa ila wananikera wavutaji njiani moshi wao nikipata hata kidogo kwa dakika zile chache nakohoa vibaya mno natamani hata Nipigie shaba hawa watu wanaovuta masihara na bangi hovyo njiani au kwenye mikusanyiko bila kujali wenzao.
 
Pilipili ni dawa nzuri Kwa kuku wenye kideli,ukitaka kuwauza unawanywesha pilipili Kwa wingi wanaamka wanachangamka Kwa kurukaruka hakuna kulala tena...atajijua mnunuaji home maana hafiki mbali anakata moto🤣🤨
 
Chakula bila pilipili naona kama chakula cha mtoto mchanga..siwezi kula kwa raha..kwangu mimi pilipili nikiungo kikubwa sana kwenye chakula kuliko hata chumvi.

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Mimi hadi najiuliza mtu unaweza kula vipi chakula bila pilipili ? kwa jinsi chakula kinavyopooza bila pilipili hata mdomoni akipandi
 

Pole sana sheikh, mie mwenyewe niliambuwa kupunguza, nikaacha kabisa miaka kadhaa hivi, nilishindwa kuvumilia especially nikiwaona wenzangu wanashushia, so nikarudia ulaji wa pilipili.

Ushauri wangu, ikiwa umezuiwa, basi acha kabisa, na ikitokea umeugua hayo maradhi, na pilipili ndio ikawa sababu ya wewe kupelekea umauti, nisiendelee, masheikh wetakuja kutueleza zaidi hukmu ya hilo, au pengine hata wewe unalifahamu sheikh wangu😅 Allah atujaalie mwisho mwema

FaizaFoxy kahtaan
 
Aamin, nimeanza kuacha siku ya 3 sasa nataka nikikishe miezi miwili kwanza.
 
Kwanijuavyo mimi pilipili ni dawa na ina faida lukuki tu kwenye afya ya binadamu, tangu nikiwa na umri mdogo sana nilikuwa nakula pilipili mpaka mama ananishangaa ila hazijawahi kunidhuru chochote hadi leo ni mtu mzima naninakula pilipili tena kwa kuitafuna yenyewe sio kuchanganya kwenye mchuzi. Tatizo lipo sehemu nyingine sema unaisingizia pilipili kwa kwa inawasha.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…