Mlioacha kutumia pilipili mliwezaje? Licha ya kunidhuru kila ninapotumia nimeshindwa kabisa kuacha ulaji wake

Mlioacha kutumia pilipili mliwezaje? Licha ya kunidhuru kila ninapotumia nimeshindwa kabisa kuacha ulaji wake

Habari za muda huu wana Jf..

Nimekuwa mtumiaji mzuri wa pilipili tokea udogoni mpaka sasa mpaka kuna kipindi nikawa ninajiuliza hivi wapi kuna mashindano ya ulaji wa pilipili na mimi nikawakilishe vizuri taifa langu ? na kwangu chakula chochote bila pilipili kwangu naona hakina maana na mzuka hauji kabisa.View attachment 2373048

Na napenda pilipili ikolee sawasawa hapo nikila stimu zipanda kichwani ubongo unachangamka mpaka nahisi pilipili inasaidia kuongeza akili maana najihusi mwepesi sana na uchangamfu wa hali ya juu wakati ninatumia.

Kiuhalisia mimi kifua changu kipo very sensitive vumbi au moshi wa sigara kidogo basi huwa nakohoa vibaya mno mpaka mwili inakoza nguvu sasa nikifululuza matumizi ya pilipili sitoboi siku tatu lazima homa ya kikohozi inapanda na madawa ya kifua mpaka nimeyazoea na hata nikiwa natumia dozi ya kikohozi bado ulaji unaendelea,kuna kipindi nilidhamiria niacha kabisa ila nilifanikiwa kujizuia kwa mwezi mmoja pekee na nimeshauriwa na wataalamu na watu wengine niache au kupunguza lakini nimeshindwa.

Kwa ambao wamefanikiwa naomba mbinu mliweza vipi kuachana na ulaji pilipili maana nataka niache kabisa kutumia.

#UziTayari
Mbona hujaomba namna ya kuacha Pombe?
 
Kwanijuavyo mimi pilipili ni dawa na ina faida lukuki tu kwenye afya ya binadamu, tangu nikiwa na umri mdogo sana nilikuwa nakula pilipili mpaka mama ananishangaa ila hazijawahi kunidhuru chochote hadi leo ni mtu mzima naninakula pilipili tena kwa kuitafuna yenyewe sio kuchanganya kwenye mchuzi. Tatizo lipo sehemu nyingine sema unaisingizia pilipili kwa kwa inawasha.

Umeenda kupima afya yako ukajua kama haijakuathiri?
 
Una uhakika pilipili ndiyo inakufanya ukohoe? Wala pilipili tuko wengi. Mimi bila kusikia ule muwasho wa pilipili chakula hakinogi. Ukinipa ugali na mboga ya majani naweza kuona ugumu kula lakini ukiongeza pilipili nakula mno. Asikudanganye mtu, pilipili ina raha zake. Nikiziona pilipili sokoni nashikwa njaa hapo hapo.
Inanoga sana hususani pale unapotupia chakula mdomoni unang'ata na kipande cha pilipili
 
Inanoga sana hususani pale unapotupia chakula mdomoni unang'ata na kipande cha pilipili
Weweee hizo ndo zangu sasa. Nikishika ile pilipili mbuzi inayonukia vizuri sana, huku kuna ugali wa nyama choma na mboga kwa mbali...
 
Na napenda pilipili ikolee sawasawa hapo nikila stimu zipanda kichwani ubongo unachangamka mpaka nahisi pilipili inasaidia kuongeza akili maana
😂😂😂Kaka hapa umetupiga kamba waziwazi
 
😂😂😂Kaka hapa umetupiga kamba waziwazi
Na hali hiyo inafanya iwe ngumu kuacha kila nikifikiria jinsi ubongo unavyokuwa stimulated kwa kasi ya ajabu naona kabisa kwenye pilipili kuna ujiniaz mwingi .
 
Na hali hiyo inafanya iwe ngumu kuacha kila nikifikiria jinsi ubongo unavyokuwa stimulated kwa kasi ya ajabu naona kabisa kwenye pilipili kuna ujiniaz mwingi .
😂😂
 
Sigara sivuti kabisa ila wananikera wavutaji njiani moshi wao nikipata hata kidogo kwa dakika zile chache nakohoa vibaya mno natamani hata Nipigie shaba hawa watu wanaovuta masihara na bangi hovyo njiani au kwenye mikusanyiko bila kujali wenzao.
We una allergy Kama Mimi mkuu, una damu group O mkuu?!
 
Na hali hiyo inafanya iwe ngumu kuacha kila nikifikiria jinsi ubongo unavyokuwa stimulated kwa kasi ya ajabu naona kabisa kwenye pilipili kuna ujiniaz mwingi .
Ingekuwa hivo wahindi wote wangekuwa majiniazi😂😂😂
 
Back
Top Bottom